Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiangalia mlango wa darasa ambao
umetengenezwa kwa mbao laini kinyume cha taratibu katika shule ya
sekondari Kasangezi kinyume chake
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akikagua ujenzi moja ya jengo katika
shule ya sekondari Kasangezi iliyoko Halmashauri ya wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma.
……………..
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametilia shaka matumizi ya fedha za
serikali zaidi ya shilingi milioni mia tano zilizotolewa kwa ajili ya
ujenzi na ukarabati wa shule ya sekondari Kasangezi iliyopo wilayani
Kasulu mkoani Kigoma.
Akizungumza mara baada ya kukagua
utekelezaji wa mradi huo waziri Ndalichako amesema shule hiyo imepatiwa
zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
4, mabweni 4 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 katika kila moja,
matundu ya vyoo 10, bwalo pamoja na ukarabati wa maabara.
Ndalichako amesema kazi iliyofanyika haiendani na fedha iliyotolewa kutokana na miundombinu hiyo kujengwa chini ya Kiwango.
“ milango ya madarasa na hata ya
mabweni mmetengeneza kwa mbao laini tofauti na BOQ pamoja na kuwa laini
ina uwazi hii nataka itolewe, tazama sakafu imeshaharibika hapa hata
mwaka haujaisha mabweni mliambiwa ya watu themanini mmejenga ya watu
sitini”
Kufuatia hali hiyo ndalichako
ameagiza kuwa ujenzi wa mabweni urudiwe kwa kuzingatia BoQ na ameaguza
ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Desemba.
“..nitakuja mwenyewe mwezi wa kwanza kukagua kama hayo yatakuwa hayajatekelezwa mengine yatafuata,”
amesema waziri Ndalichako.
Aidha waziri Ndalichako amemuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya
kumuondoa mara moja shuleni hapo mkuu wa shule hiyo kwa kushindwa
kusimamia vizuri kazi hiyo na hivyo kuisababishia hasara serikali.
“Kwanza ujenzi wa mara ya kwanza
hata matofali hukununua ulichukua kwenye benki ya wananchi na tayari
nilikuwa nimeleta fedha sasa kwanini hukujiongeza hata ukarekebisha
ofisi ya Mkuu wa Shule ambayo iko katika hali isiyoridhisha vitu vingine
ni kudhalilisha Serikali, Mkurugenzi muahamishe huyu katika shule hii,”
alisema waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako pia ameitaka
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kasulu
kufuatilia muenendo wa upatikanaji wa madawati miamoja themanini
yaliyonunuliwa katika mradi huo kama yametimia na yamenunuliwa kwa
kufuata utaratibu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kasulu Kanali Saimon Anange amekiri kuwepo uzembe katika kusimamia
miradi hiyo na kumuhakikishia waziri Ndalichako kuwa ofisi yake
itafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa katika ziara hiyo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolijia Prof. Joyce Ndalichako
yupo mkoani Kigoma Kwa ziara ya Kikazi akikagua miradi ya elimu
inatekelezwa kupitia fedha za Programu ya lipa kwa matokeo EP4R.
0 comments:
Post a Comment