Mkuuwa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema aliye vaaqkilemba ,aliye upande waq kushoto ni Diwani wa kata ya Ilala Mhe. Saad Kimji akifagia na vijana wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Ilala katika Hospital ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo katika kuelekea madhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Mwalimu JK nyerere.
Mmoja wa viongozi wa umoja wa vijana CCM ilala akimpati zawadi ya Sabuni mama mzazi Ruth Eliya aliye jifungua jana katika Hospital ya mnazimoja ,aliye upande wamisho kulia ni Mkuuwa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema .
Diwani wa kata ya Ilala Mhe.Saad Kimji akizungumzaz na waandishi wa habari baada ya zoezi la kufanya usafi na kutoa misaada katika hospital ya mnazi mmoja
Katibu wa umoja wa vijana UVCCM Wilaya ya Ilala Irene Moleli akizungumza na wana habari baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi na kutoa misaada katika hospital ya Mnazi mmoja , moja ya misaada ilitolewa hapo ni sabuni ya unga na sabuni za mche.
Mganga mfawidhi wa Hospital ya mnazi mmoja Helman Ngonyani, akitoa neno la shukrani kwa UVCCM na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuhitika kwa ziara hiyo.
Baadhi ya vijana wa UVCCM wakizoa taka katika Hospital ya Mnazi mmoja ,
Baadhi ya vijana wa UVCCM wakizoa taka katika Hospital ya Mnazi mmoja ,
Na Mwandishi wetu Dar
Katika kuazimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ameongoza umomoja wa Vijana CCM, Wilaya ya Ilala kufanya usafi na kugawa misaada ya kijamii katika Hospital ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mhe. Mjema amesema , Wameamua kufanya usafi na kugawa zawadi hizo ili kumuenzi Babawa Taifa na amewapongeza vjiana wote walijitokeza katika shuguli hiyo kwani nitendo la uzalendo amabalo linawafanya watu wengi kumkumbuka mwalimu Nyerere kwa uadilifu wake alivyo litumika Taifa enzi ya uhai wake.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospital hiyo Helmani Gonyani, amewashukuru vija wa umoja huo kwa kutembelea hospitali hiyo na kufanya usafi na kuwataka tena iwapo wata pata nafasi siku nyingine wafanye hivo kwani wamefariji wagonjwa na kuhamasisha umoja wa kitaifa.
Naye diwani wa kata ya Ilala Saad Kimji akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa kata hiyo ameushukuru uongozi wa hospital hiyo kwa mapokezi na ushirikiano wa walioupata katika hospital hiyo na kupongeza watumishi wote wa hospital kwa uzalendo wao na kutoa huduma kwa , na kutoa wito kwa vijana wa Illala kuwa wazalendo kwa kufanya kazi za kijaamii bila kujali itikadizao za kisiasa.
Irene Godfrey Moleli ni katibu wa umoja wa vijina wa wilaya ya Ilala , amesema , UVCC Wilaya hiyo umeandaa bonanza na ligi ya mpira kwaajili ya kumuenzi hayati Mwalimu Julias Nyerere ambapo itaanza tarehe 21 hadi 28 mwezi kakatika jimbo la Segerea na amewakaribisha vijana wote kuhudhuri uzinduzi wa ligi hiyo na kushiriki michezo kwa muda wote wa ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment