METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 14, 2017

KATIBU MWENEZI WA CCM MANISPAA YA IRINGA WAPINZANI MJIPANGE VILIVYO KUENDELEA KUWA MADARAKANI

 Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo sabasaba manispaa ya Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.


Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kujipanga vilivyo kwa kuwa amechaguliwa kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi na wananchi wa manispaa wanakuwa na imani na kukirudisha chama hicho madarakani katika chaguzi zote zitakazo jitokeza hapo baadae.

Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Bashir alisema kuwa atahakikisha anakieneza chama vilivyo ili kuongeza wanachama wanaokipenda chama hicho.

“Mimi mwenezi hivi nilivyo nitakieneza chama kwa nguvu zote kwasababu tunavijana na viongozi wa kuleta mabadiliko ndani ya chama hata mkisema ninyoe nywele nitanyoa(hata wakisema tumooge mafwiri tumoga eeela) kwa lengo la kuhakikisha tujakijenga chama kuwa chama cha wananchi” alisema Bashir

Bashir aliwataka wanachama kushikana kuahakikisha wanakuwa wamoja ili kuongeza wanacha wengine na kuendelea kuimalisha jumuhiya zote za chama hicho za  manispaa ya Iringa.

“Bila kuwa na umoja hatuwezi kwenda mbali wala kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mmenichagua kuwa mwenezi hivyo nitaifanya kazi yangu kwa moyo wangu wote” alisema Bashir

Aidha Bashir aliwashukuru wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa na imani naye na kuhakikisha amekuwa mwenezi hivyo ametoa pongezi kwa wale waote waliomchagua kwa kura nyingi.

“Mmenifanya niwe na furaha sana maana sio kwa wingi wa zile kura mlizonipa  na kunifanya leo hii nasimama kama mwenezi kwa ajili ya kura zenu sasa subirini kazi yangu ya kukieneza chama na naomba tusahau yote yaliyopita na kuhakikisha tunaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Bashir

Naye katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marko Mbago alimpongeza Edwin Bashir kwa ushindi alioupata na kumuomba kukieneza chama kwa nguvu zote hata kwa kuutumia umaarufu wake kuongeza wanachama ambao watakitumikia chama hiki hapa manispaa.

“Wewe ni maarufu na unapendwa sana hivyo tunatengemea mengi kutoka kwa kutokana na uzoefu wako wa kuishi vizuri na wananchi wa manispaa ya Iringa na kuijenga CCM mpya hapa manispaa” alisema Mbago

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa sasa ni muda mwafaka wa kuongeza wanachama wapya na kuimarisha jumuhiya zote hapa manispaa ili kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kushinda tena.

“Mimi nakufahamu muda mrefu sasa tumia vijana wako wote ambao umewapa mafanikio kwa muda mrefu kukurudisha fadhila na kukuunga mkono katika harakati zako za kisiasa” alisema Rubeya

Ritta Kabati ni mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alimpongeza mwenezi Edwin Bashir kwa ushindi alioupata lakini akawataka viongozi wengine kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika haraka zake za kueneza chama.


“Kufanya kazi pekee yake hawezi kupata matokeo chanya hivyo ni lazima sisi viongozi na wanachama kumpa ushirikiano wakutosha kuhakikisha mikakati yake inaenda vile chama kinataka na kuahikisha anaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Kabati
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com