Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Ali Ahmadov wakati
alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heydar Aliyev, Oktoba
25, 2019 amabako atamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye
mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote unaofanyika Baku nchini
humo.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
……………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo
Oktoba 26, 2019 anatarajiwa kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli
katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi
zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko
duniani utakaofanyika Baku, Azerbaijan.
Mkutano huo unalenga kujadili
namna ya kutatua changamoto za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazokabili
nchi wanachama wa NAM katika nyakati za sasa, pamoja na na kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi wanachama wa umoja huo.
Waziri Mkuu aliwasili nchini
Azerbaijan jana (Ijumaa, Oktoba 25, 2019) na alipokelewa na Naibu Waziri
Mkuu wa Azerbaijan, Bw. Ali Ahmadov pamoja na viongozi wengeine wa
Serikali hiyo. Mapokezi hayo yalifanyika katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Heydar Aliyev.
Ajenda za mkutano huo ni
kupokea ripoti za mkutano wa maandalizi wa Mawaziri, kupokea ripoti ya
mkutano wa maandalizi wa Maafisa Waandamizi, uchaguzi wa nchi
zitakazokuwa wajumbe katika ofisi ya uratibu wa shughuli za NAM, New
York kwa kipindi cha mwaka 2019-2022.
Mbali na ajenda hizo, pia
ajenda nyingine za mkutano huo ni kupokea ripoti za shughuli za umoja
huo zilizotekelezwa chini ya Mwenyekiti wa NAM, Venezuela, mjadala mkuu,
pamoja na kupitisha maandiko yatokanayo na mkutano.
Mheshimiwa Majaliwa
ameambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika ya
Mashariki, Dkt. Damasi Ndumbaro na Balozi wa Tanzania Nchini Urusi
ambale pia ni Balozi wa Azerbaijan, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi.
Awali, Waziri Mkuu alikuwa
Sochi nchini Urusi ambako pia alimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli
katika Mkutano wa Uchumi kati ya Urusi na Afrika (Russia – Africa
Economic Forum) na baadae Mkutano wa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Mataifa ya Afrika uliofunguliwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
0 comments:
Post a Comment