Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya KIlimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa (Kushoto) na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa (Kulia) mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi huo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Lupa na Meneja wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga Ndg Abdillah Nyangasa sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa NFRA mara baada ya kutembelea Ofisi za NFRA kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Katavi
Waziri
wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa
maghala na vihenge vya kisasa kanda ya Sumbawanga kuongeza kasi ili kukamilisha
haraka mradi huo kwa mujibu wa makubaliano.
Alisema
kuwa kampuni iliyoteuliwa baada ya kushinda zabuni kwa ajili ya ujenzi wa mradi
huo ni UNIA ARAJ REALICZJE ya nchini Poland ambayo ilimteua mkandarasi msaidizi
mzawa anayejulikana kwa jina la ELERAI CONSTRUTION CO. LTD wa Arusha, hivyo
napaswa kuongeza kasi ya ujenzi kutokana na kasi iliyopo kwa sasa kutoridhisha.
Waziri
Hasunga ameyasema hayo juzi tarehe 10 Octoba 2019 mara baada ya kutembelea ujenzi
wa mradi huo kwenye Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi utakaowanufaisha wakulima
wa mazao ya nafaka kwani serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) pamoja na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) itakuwa na uwezo wa
kununua mazao mengi kwa wakulima na kuyahifadhi kwa muda mrefu.
Alisema
kuwa kampuni hiyo inayojenga vihenge vya kisasa na miundombinu mingine ikiwemo maghala
katika eneo la Kanondo Manispaa ya sumbawanga mkoani Rukwa na Mpanda Mkoani
Katavi bado haijamfurahisha kutokana na kasi ndogo ya ujenzi wa mradi.
Mhe
Hasunga amesema kuwa serikali imekusudia kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka
nchini ili kuwanufaisha wakulima punde wanapovuna mazao yao hususani nafaka
kwani kufanya hivyo wakulima wataongeza uzalishaji na tija kwenye mazao na
kuliongezea Taifa pato kubwa.
Alisema
kuwa vihenge hivyo vitakuwa na uwezo wa kuhifadhi jumla ya Tani 20,000 za
nafaka huku ujenzi wa miundombinu mingine ukiendelea kama jingo la Ofisi ya
utawala, Ghala la kawaida la ujazo wa Tani 5000 za nafaka, na Mzani mkubwa wa
daraja (Electronic weighbridge).
Mradi
huo utakuwa na gharama ya Dola za kimarekani 6,019,399 ambazo ni takribani
shilingi za Kitanzania Bilioni 14 kwa mradi wa eneo la Kanondo Sumbawanga na
vilevile Dola za Kimarekani 6,180,857 sawa na fedha za kitanzania Shilingi Bilioni
14.2
Mhe
Hasunga ametilia nyundo kuwa serikali haitaongeza muda kwa mkandarasi endapo
atashindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.
Muda
wa mradi kuanza hadi kukamilika ni jumla ya miezi 18 (Mwaka mmoja na nusu), Kwa
upande wa Mpanda mkoani Rukwa mradi umeanza tarehe 14 Januari 2019 na umepangwa
kukamilika tarehe 14 Julai 2020 wakati upande wa Kanondo mkoani Katavi mradi
huo umeanza tarehe 8 Septemba 2019 na unatarajiwa kukamilika tarehe 8 Machi
2021.
Punde
mradi huu utakapokamilika mkoa wa Rukwa utakuwa na Maghala ya Wakala wa Taifa
wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka za Tani 58,500
wakati mkoa wa Katavi utakuwa na uwezo wa kuhifadhi Tani 28,000 ikihusisha pia
maghala ya zamani.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment