Baadhi ya wauguzi wakishangilia
wakati Mgeni rasmi akiingia ukumbi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019
ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019
ambao unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifungua Kongamano la
kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, kwa niaba ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi
Mkoani Simiyu.
Rais wa Chama cha Wauguzi nchini,
Bw. Paulo Magesa akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi na Mkutano
Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao unafanyika
kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa
Simiyu(kushoto) na viongozi wa Chama cha Wauguzi Tanzania bara
wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na
Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao
unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu wa Chama cha Wauguzi
nchini, Bw. Sebastian Luziga akisoma risala ya wanachama kwa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Kongamano la kisayansi na
Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, 01 Oktoba, 2019 ambao
unafanyika kwa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wauguzi wakiwa katika
maandamano ya amani 01 Oktoba, 2019 kuelekea ukumbi wa Shule ya
Sekondari Kumbukumbu ya Kusekwa mjini Bariadi, mahali ambapo Kongamano
la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 47 wa Wauguzi Tanzania Bara, ambao
unafanyika kwa siku nne Mkoani Simiyu.
Wauguzi wakicheza wakati muuguzi
mwezao akitoa burudani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kisayansi na
Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara 01 Oktoba, 2019 ambao
unafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania Bara wameomba Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini(TNMC)
kupunguza gharama za ada ya leseni za uuguzi ambazo wamedai kuwa ni
kubwa na zinaathiri vipato vyao.
Ombi hilo limetolewa na Katibu
wa Chama cha wauguzi Tanzania Bara(TANNA) Bw. Sebastian Luziga wakati
akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
alipofungua Kongamano la kisayansi na Mkutano wa 47 wa wauguzi kwa niaba
ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Oktoba 01, 2019 Mjini Bariadi.
Luziga amesema awali ada hiyo
kwa ngazi ya astashahada ilikuwa 20,000/= stashahada na shahada na
shahada ya uzamili ilikuwa shilingi 40,000/=, hivi sasa kumekuwa na
ongezeko kubwa la ada ambapo astashahada wanapaswa kulipa shilingi
40,000/=, stashada 60,000/=shahada 80,000 na shahada ya uzamili na
uzamivu ni 120,000/=.
“Ongezeko hili ni kubwa na
linaathiri sana kipato cha wauguzi kwani hakuna uwiano kati ya kupanda
huko kwa ada na ongezeko la mshahara; kupitia Wizara ya Afya tunaomba
lishughulikiwe upya kwa kufuata utaratibu wa kushirikisha wadau,”
alisema Luziga
Akizungumza mara baada ya
kupokea risala hiyo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameahidi
kulifikisha suala hilo pamoja na mengine yaliyowasilishwa kwa Waziri wa
Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, huku akiwaomba viongozi kulitafakari kwa upya
ongezeko la ada wakizingatia hali halisi ya mishahara ya wauguzi, kodi
na makato na waone busara kama ipo haja na hoja ya kuongeza ada hiyo.
“Suala hili ni hoja ya walio
wengi, ninyi nyote mmemuona Mhe. Rais akizungumzia kuondolewa kwa tozo
nyingi zisizo na sababu kwenye kilimo, mifugo, uvuvi; hata hili la kwenu
linaweza kusababisha serikali iwe na nia ya kufahamu mabaraza yake yote
na tozo zao, nawaomba viongozi mlitafakari muone kama ipo hoja na haja
ya kuongeza gharama za ada,” alisema Mtaka.
Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa
Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema mkoa unatambua kazi inayofanywa na
wauguzi ya kutoa elimu kwa wajawazito na kuhamasisha wajifungulie
kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo mwaka 2017 wanawake
waliojifungulia kwenye vituo vya afya ni asilimia 55 na mwaka 2018
ikapanda kufikia asilimia 70.
Naye Afisa Muuguzi kutoka
Halmashauri ya Ubungo Bi. Aliho Ngeregenza amesema wauguzi walio wengi
vipato vyao wanavyopata haviendani na gharama za leseni wanazolipia
hivyo ombi lao wapunguziwe gharama hizo
Kongamano la Kisayansi na
Mkutano Mkuu wa 47 wa wauguzi Tanzania Bara ambalo linahusisha wauguzi
zaidi ya 800 litafanyika kwa muda wa siku nne Mjini Bariadi mkoani
Simiyu.
Kulingana mishahara kutoongezewa ni ukweli mtu tupunguziwe Ada hizo
ReplyDelete