Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na wananchi wa Baleni wilayani Mafia mkoa wa Pwani
alipokwenda kusikiliza kero za ardhi katika eneo hilo akiwa katika ziara
yake ya siku mbili katika wilaya hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli
ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi
jana.
Mwananchi
Hassan Omar maarufu mzee wa Lumbesa mkazi wa Dagoni Mafia akimuonesha
nyaraka Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula kuhusiana na mgogoro wa ardhi wakati Dkt Mabula alipofanya ziara
wilaya ya Mafia kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akikagua Majalada ya Ardhi katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mafia jana wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya
ardhi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnenduma na Kulia
ni Afisa Ardhi Chuchu Ochere.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akiangalia baadhi ya Nyaraka za umiliki wa ardhi kutoka kwa Hassan
Mohamed (Kushoto) na Mwanangano Mohamed wakati wa ziara yake ya kutatua
migogoro ya ardhi katika wilaya ya Mafia jana (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
…………………………
Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda
kuyavunja Mabaraza yote ya Kata na Vijiji ya ardhi yasiyotenda haki
wakati wa kutoa maamuzi katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani.
Dkt
Mabula alitoa agizo hilo jana akiwa katika ziara yake ya siku mbili
wilayani Mafia mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali
kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi.
Alisema,
kutokana na kero nyingi za ardhi alizozipokea katika ziara yake hiyo
wilayani Mafia amebaini Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya hiyo
hayafanyi kazi zake vizuri na wajumbe wake wamekuwa wakiyatumia kutoa
maamuzi yasiyotenda haki.
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, kadri Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya ya
Mafia yanavyofanya vibaya katika utoaji maamuzi yake basi hata
uanzishwaji Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya hiyo halitafanya vizuri
katika utendaji wake.
‘’Ukiwa
na watu wasioweza kusimamamia haki itakuwa shida sana, Mkurugenzi
hakikisha Mabaraza ya Ardhi katika Kata na Vijiji yasiyofuata taratibu
na kutoa haki kwa walalamikaji unayavunja na kuteua wajumbe wapya’’
alisema Dkt Mabula.
Naibu
Waziri wa Ardhi alitaka kupitiwa upya Mabaraza yote ya ardhi ya Kata na
Vijiji katika wilaya ya Mafia hasa yale yanayolalamikiwa na kubainisha
kuwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko tayari kutoa
Msajili wa Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba nchini ili atoe elimu katika
Mabaraza hayo kwa lengo la kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Alisema,
Mabaraza ya ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia hayatendi
haki na wakati mwingine Baraza la Kata linachukua kesi ya Baraza la
Kijiji lengo likiwa kutotenda haki kwa walalamikaji.
Baadhi
ya wananchi wa Mafia wamelalamikia Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji
katika wilaya ya Mafia mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi kuwa wajumbe wake
hawatendi haki wakati wa kutoa maamuzi na hivyo kuonesha dhahiri uwepo
dalili za rushwa.
Mohamed
Shaban alimueleza Dkt Mabula kuwa, Mabaraza ya ardhi ya Kata wakati
mwingine hayatendi haki na kumtaka anayeshindwa kesi kwenda Baraza la
Ardhi la Nyumba la wilaya la Mkuranga huku wakijua mlalamikaji
atashindwa kwenda Mkuranga kutokana na changamoto za usafiri na hivyo
kupoteza haki yake.
Awali
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda alieleza
kuwa Mabaraza ya ardhi ya Kata na Kijiji katika wilaya hiyo yapo na
yanafanya kazi na wajumbe wake wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ingawa
alieleza changamoto iliyopo Baraza katika kata ya Kilindoni ambalo
alilileleza kuwa badala ya kuatatua matatizo limekuwa chanzo cha
migogoro kwa kuwa wakati mwingine hufanya mashauri yaliyo nje ya kata
yake na suala hilo tayari alishalitolea agizo la kuvunjwa kwa baraza
0 comments:
Post a Comment