Umoja
wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa uchaguzi
mjini Aschaffenburg Ujerumani jumamosi 28.09.19. Katika uchaguzi huo
watanzania wanaoishi ujerumani walichagua viongozi wapya, nafasi ya
mwenyekiti alichaguliwa Mwl. Bi Upendo Vanessa Lyimo Foelesen kuwa
mwenyekiti wa UTU e.V, baada ya mwenyekiti mstaafu Bw. Mfundo Peter
Mfundo kukataa kugombea nafasi hio, ambayo amekaa kwa muda wa miaka 9,
na kukitumikia chama hicho kwa muda wote huo, hata hivyo kamati
ilimuomba achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamati, mshauri, mlezi wa
UTU e.V na kiongozi muandamizi katika shughuli za UTU e.V
Watanzania wanaoishi ujerumani waliwachagua viongozi wafuatao.
Mwenyekiti: Mwl. Bi Upendo Vanessa Lymo
Makamo Mwenyekiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo
Katibu: Bi. Petrida Karch
Muweka hazina: Bw. Mngoya Lukuta
Wanakamati:
Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw. Ebrahim Makunja (aka Kamanda Ras Makunja)
Bw. Sudi Mnette
0 comments:
Post a Comment