
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya
wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya
Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba,
yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya
wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS)
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama
vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na
Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019
Mjini Bariadi.Oktoba 18, 2019.

Baadhi ya
wakulima na Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS)
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama
vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na
Kutunza Kumbukumbu za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019
Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za Chama, wakati wa
uuzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu
za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa neno la shukrani wakati wa
uzinduzi wa mafunzo ya wakulima na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) juu ya Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu na Kutunza Kumbukumbu
za Wakulima wa Pamba, yaliyofanyika Oktoba 18, 2019 Mjini Bariadi.
……………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkoa wa Simiyu umeanzisha mfumo
rasmi wa ukusanyaji takwimu na utunzaji wa kumbukumbu za wakulima wa
pamba uitwao ‘Kilimo Maendeleo’ utakaowawezesha wakulima kusajiliwa
katika Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS), kuuza pamba yao kwa njia
ya mtandao na kupata pembejeo zote kutoka kwa wauzaji wa pembejeo.
Akizungumza katika uzinduzi wa
mafunzo juu ya mfumo huo, Meneja wa huduma za ugani kutoka GATSBY
AFRICA, Bw. Sunday Mtaki amesema Mfumo huo utaanza kutekelezwa katika
AMCOS 24 zilizoteuliwa kwa kuanzia.
“Katika utekelezaji wa mkakati
wa miaka mitano ya mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, eneo la usajili
wa wakulima na matumizi ya TEHAMA kwenye kilimo ni muhimu sana,
tumeileta kampuni inaitwa LITENGA ambayo ina mtandao unaitwa Kilimo
Maendeleo kazi yake ni kuwaunganisha wakulima kupitia AMCOS na taarifa
zote za mkulima zitapatikana kupitia simu za mkononi,” alisema Mtaki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema
mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa
kilimo cha zao la pamba ulioandaliwa na Mkoa kwa kushirikiana na wadau,
kwa lengo la kuboresha kilimo cha pamba, huku akiwataka Maafisa Kilimo
na Maafisa ushirika kutimiza wajibu wao.
“Maafisa Kilimo na Maafisa
Ushirika timizeni wajibu wenu msisubiri mgombane na mtu hii kazi ndiyo
inayowapa heshima, Serikali ya Rais Magufuli imeweka mkakati wa
kuhakikisha zao la pamba linakuwa zao muhimili kwenye nchi yetu, ndiyo
maana sisi kama Mkoa tumeanza utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano wa
kilimo cha zao la pamba,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ameongeza kuwa
dhamira ya mkoa ni kufanya mapinduzi katika kilimo cha pamba ili
wakulima walime kilimo cha kisasa chenye tija na kuwa na ushirika imara,
ambapo amesema viongozi wa AMCOS wasio waaminifu watachukuliwa hatua
kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika
cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Charles Madata amewaonya viongozi wa
AMCOS kuwa waaminifu na kuhakikisha kila mmoja anakuwa na nidhamu ya
fedha ili mali za wakulima ziweze kuwa salama.
Kwa upande wake Kaimu Mrajisi wa
Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu amesema viongozi
wote wasio waaminifu watachukuliwa hatua, ambapo amebainisha kuwa
takribani viongozi 107 wa AMCOS wilayani Maswa waliohusika na ubadhilifu
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa
ukaguzi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema kupitia mkakati wa miaka mitano ya
mkoa wa Simiyu katika zao la pamba, mkoa wa huo unatarajia kuongeza tija
ya uzalishaji wa pamba kutoka kilo 200 kwa ekari hadi kufikia kilo 600
hadi 1000 au zaidi kwa ekari.
0 comments:
Post a Comment