METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 21, 2016

Obama asikitishwa na malalamiko ya Trump


Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barack Obama wa Marekani ameyaelezea malalamiko yaliyotolewa na mgombea kupitia chama cha Republican, Donald Trump, kwamba kuna udanganyifu unafanyika katika uchaguzi wa Rais nchini humo, kuwa ni ya hatari na kuharibu demokrasia.

Amemlaumu mgombea huyo wa Republican kutilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, bila ya kuwa na ushahidi kamili wa kuwepo kwa hila kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Wakati wa mdahalo wao wa tatu na wa mwisho uliofanyika jana katika yake na mpinzani wake Hillary Clinton, Bwana Trump alikataa moja kwa moja kusema kwamba atakubali matokeo iwapo atashindwa.

Hata hivyo chama chake cha Republican kimekuwa kikijaribu kusafisha kauli yake hiyo.

Timu ya Kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump inamlaumu Hillary Clinton mgombea kupitia chama cha Democrats kwa kupanga jaribio la kutaka kumchafua mgombea huyo wa Republican baada ya mwanamke wa 10 kujitokeza akiilaumu tabia yake ya kudhalilisha wanawake kijinsia.

Mwana mama huyo Karena Virginia anamtuhumu Bwana Trump kwa kile alichosema alimpapasa kifuani, wakati wa mashindano ya mchezo wa tenisi mwaka 1998.BBC
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com