METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 19, 2019

Wazazi Mkoani Mwanza Watakiwa kuwapeleka Watoto kupata Chanjo

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella
amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka
mitano kwenye Vituo vya Afya kupata chanjo bure hidi ya magonjwa ya Surua,
Rubella na Polio kuanzia tarehe 17-21 Oktoba 2019.
 
Kwa Mkoa Mwanza, zaidi ya watoto laki
sita (watoto 637,579) wanatarajiwa kupewa chanjo ya Rubella na Polio huku
watakaopewa chanjo ya Surua wakitarajiwa kuwa zaidi ya elfu sitini (watoto
266,140) hivyo kufanya jumla ya watoto wanaotarajiwa kuchanjwa kuwa laki tisa
elfu tatu  mia saba kumi na tisa (watoto
903,719). 
Kitaifa uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika mkoani Morogoro, Oktoba 17,
2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Surua, Rubella na Polio.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akitoa salamu za Wizara kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo mkoani Mwanza.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com