METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, October 7, 2019

RC Mongella atoa maelekezo kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewataka Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza, kuhakikisha wanatimiza vyema wajibu wao ili zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la wakazi wenye sifa za kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lifanyike kwa amani.

Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ameyasema hayo Oktoba 07, 2019 kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza na kubainisha kwamba zoezi hilo linatarajiwa kuanza Oktoba 08, 2019 (mwisho Oktoba 14, 2019) huku Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com