*****************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa
Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya
mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na
kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na
gharama za usafiri.
RC Makonda amesema ameamua
kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa
wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya “Njoo Kesho”
pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.
Aidha RC Makonda amebainisha kuwa
mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji
wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa
zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya
husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.
Hata RC Makonda amewahimiza
wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo
Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa
taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.
Jinsi kuwasilisha ujumbe andika
neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au
ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa
mara moja na kupewa mrejesho.
0 comments:
Post a Comment