Na Innocent Natai,
TPRI-Arusha
Kaimu Mkurugenzi
mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda
wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) Dkt Margaret
Mollel amewataka wauzaji na wasambazaji wa viuatilifu nchini kuepuka
uuzaji wa viuatilifu ambavyo vinaingizwa kwa njia za panya ambavyo havijakaguliwa
na kusajiliwa na taasisi hiyo.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu inayofanyikia katika taasisi hiyo mkoani
Arusha, ikiwa kutanisha watafiti wanaofanya majaribio ya kuhakiki
viuatilifu kabla ya kuvisajili kutoka katika vituo vya kilimo hapa nchini kutoka
SUA pamoja na TPRI kadhalika wataalamu waliobobea katika maeneo hayo ili
kuondoa changamoto ya uandaaji wa ripoti.
Dkt Mollel
ametoa mwito kwa wafanyabiashara wa viuatilifu kuacha Kufanya biashara bila
kibali, Kuuza/kusambaza
viuatilifu visivyosajiliwa, Kuuza /kusambaza viuatilifu visivyo na vibandiko
(lebo), Kuuza
viuatilifu vilivyoisha muda wa matumizi, na Uhamishaji wa viuatilifu (Repacking/Decanting)
Kuuza
viuatilifu kwenye eneo ambalo halijakaguliwa na Mkaguzi wa Viuatilifu, Kuuza viuatilifu kwa kutembeza mitaani, Kuuza
viuatilifu kwenye masoko, minadani na kutandaza barabarani/vijiweni kwani
hayo makosa yote yanaweza kuwasababishia wakulima hasara kwa kununua viuatilifu
ambavyo havikidhi haja yao na wakati mwingine kuleta madhara katika mazao,
mazingira na hata kwa binadamu.
Aidha
amewaasa pia wakulima kuacha kununua viuatilifu ambavyo vinaingizwa hapa
nchini kinyume na sheria vikiwa havijafanyiwa utafiti na kusajiliwa na TPRI
kwa kisingizio cha kupunguza gharama kutokana na wahalifu hao kuuza kwa
bei rahisi.
“Tunataka
viuatilifu vilivyo bora hapa nchini, wachukue viuatilifu vyenye nembo ya TPRI
ambavyo tumeshakwisha kuvifanyia utafiti, kuvikagua na kuhakiki kuwa havina
madhara tuna wataalamu waliobobea ambao wanapima viuatilifu kabla ya kuvisajili
kwa ajili ya kutumika hapa nchini hivyo mmavyo nunua kwa bei rahisi havina
ubora uliokusudiwa utanunua vingi na bado hautaweza kuuwa visumbufu “ Alisema Dkt
Mollel
Pia amesema kuwa
watakao kutwa wakiuza au kuvisambaza viuatilifu ambavyo havija fanyiwa utafiti,
kukaguliwa na kusajiliwa na TPRI (ambavyo havina nembo ya TPRI) na makosa hayo
mengine watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo Faini: Kati ya Shilingi milioni
10 hadi milioni 100 kwa makampuni makubwa, mtu binafsi
faini Kati ya Shilingi milioni 2 hadi milioni 10 au
kifungo miaka mitatu au vyote, kwa mkosaji sugu adhabu zilizotajwa hapo juu
pamoja na kunyang’anywa kibali cha kufanya biashara ya viuatilifu.
Aidha
akizungumzia warsha hiyo inayofanyikia katika taasisi hiyo ikiwakutanisha
watafiti wanaofanya majaribio ya kuhakiki viuatilifu kabla ya
kuvisajili kutoka katika vituo vya kilimo hapa nchini, SUA, TPRI na wataalamu
waliobobea katika maeneo ya viuatilifu.
Amesema kuwa
warsha hiyo imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuondoa changamoto iliyokuwepo
katika uandaaji wa ripoti za utafiti ili kukaa pamoja na kuwekeana utaratibu na
mwongozo wa namna gani wataandaa ripoti zilizo katika mfumo mmoja pia kwa
kufuata miongozo iliyowekwa kwa nchi za jumuia ya Afrika Mashariki.
“Baada ya
warsha hii watatoka na mfumo mmoja katika uandaaji wa ripoti, na sio kwamba
hapo nyuma walikuwa wanafanya vibaya hapana walikuwa wanafanya vizuri” Aliongeza Dkt
Mollel
Ametoa wito
kwa washiriki wote wa warsha hiyo elimu watakayo ipata waipeleke kwa wengine
ambao hawajafanikiwa kushiriki na pia watoke na azimio moja zuri kwas ababu
itarahisisha katika vikao vya kupitisha viuatilifu kabla ya usajili.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment