![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/b6896d0206e661afe783637da914ddda.jpg)
*********************************
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameahirisha
sherehe za maadhimisho siku ya Makazi Dunia na kuagiza fedha iliyopangwa
kwa ajili ya sherehe hiyo shilingi milioni 23 kutumika kuboresha mfumo
wa mapato na utoaji huduma za ardhi.
Katika
salamu zake za siku ya Makazi Duniani yenye kauli mbiu ‘Matumizi ya
Teknolojia Bunifu Kubadili Taka kuwa chanzo cha Mapato’ Lukuvi ametaka
maadhimisho ya mwaka huu kutofanyika sherehe na badala yake yatumike
kutafakari kauli mbiu ya na kujipanga upya kutekeleza agizo la rais
alilolitoa muda mrefu la kuwataka wananchi kujitolea kufanya kazi za
usafi katika maeneo ya miji na wanayoishi.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kauli mbiu ya
maadhimisho ya mwaka huu inaelekeza kutafakari kwa kina namna changamoto
ya uwepo wa taka mijini kuwa fursa ya kujiongezea kipato kwa kutumia
teknolojia rahisi.
Alisema,
mwaka huu inaelekezwa kuingia kwa undani zaidi kutumia ubunifu kubadili
taka kuwa mtaji na kuongeza kipato kwa wananchi bila kuathiri afya za
wakazi wa mijini na mazingira na hatimaye kupunguza gharama za udhibiti
taka.
‘’Mamlaka
za miji zina wajibu wa kukusanya taka kama mojawapo ya huduma
wanazotakiwa kuzitoa kwa wananchi na kwa upande mwingine wananchi wanao
wajibu wa kulipia huduma hiyo kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha mamlaka
za mitaa’’ alisema Lukuvi.
Aliwaasa
wananchi kuepuka kutupa taka kando ya mito , maeneo ya wazi ,
barabarani na katika mitaro ya maji ya mvua kwa kuwa kufanya hivyo
kunasababisha uharibifu wa mazingira , kuziba kwa mitaro ya maji ya
mvua na kutengeneza mafuriko.
Aidha,
ameaalika wadau wote wenye teknolojia rahisi ya kuchakata taka ngumu
kushirikiana na mamlaka za miji nchini ili kutumia ujuzi huo kupambana
na changamoto ya wingi wa taka ngumu na kwa njia hiyo wataweza
kutengeneza ajira kwa jamii huku miji ikiendelea kuwa safi na afya za
wananchi kuimarika.
Shirika
la Umoja wa Mataifa linalosimamia Makazi Duniani (UN Habitat) kupitia
azimio Namba 40/202 la Baraza la Umoja wa Mataifa la mwezi Desemba mwaka
1985 limetenga jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ya kila mwaka kuwa
siku ya Makazi Duniani. Kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yalifanyika
jijini Nairobi, Kenya mwaka 1986. Mwaka huu Maadhimisho hayo yanafanyika
kimataifa katika jiji la younde Cameroun.
0 comments:
Post a Comment