Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa
pili kulia) akioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma mkoa wa Mara jana wakati wa
ziara yake mkoani humo. Mradi huo unajengwa na Shirika la Nyumba la
Taifa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa
pili kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya
ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa
Musoma mkoa wa Mara jana. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Mara
Carlone Mtapula.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa
pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Ubunifu Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) Magret Ezekiel (kulia) kabla ya kuanza kufanya
ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa
Musoma mkoa wa Mara jana. Wa pili kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Carlone Mtapula.
………………….
Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Ujenzi
wa Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwanga iliyopo Musoma mkoa wa Mara
unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kugharimu zaidi ya
shilingi Bilioni 15 unatarajiwa kukamilika Agosti 2020.
Hayo yameelezwa jana mjini Musoma na Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Margret Ezekiel wakati
akitoa taarifa ya maendeleo ya uendelezaji ujenzi wa mradi wa hospitali
hiyo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo,
Margret
alisema, jengo hilo lenye mita za mraba 24482 na majengo mengine ya
pembeni yenye mita za mraba 1039 lina sehemu kuu tatu zinazojumisha
sehemu zenye ghorofa tano, nne na sehemu ya tatu ghorofa mbili.
Alisema,
ujenzi wa mradi wa hospitali ya Kwangwa ulianza septemba 2019 na
kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa mradi huo kulitokana na changamoto ya
upatikanaji wa michoro ya kujengea pamoja na kutokamilika kwa mchakato
wa kumpata Mshauri Mwelekezi wa mradi.
‘’jengo
hili ambalo limepitia wakandarasi wawili kabla ya shirika letu
kukabidhiwa limefanyiwa maboresho ili kuwa na huduma zote kadri ya
hospitali ya Rufaa inavyotakiwa’’. Alisema Margaret
Kwa
mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo Ubunifu wa NHC, kazi za ujenzi
zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kupiga lipu katika katika maeneo
yote ambayo hayatakuwa na marejkebisho , kuvunja baadhi ya kuta na
kuzijenga kwa mujibu wa marekebisho sambamba na kuandaa sehemu ya
nyongeza,
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula alisema kukamilika kwa jengo la hospitali ya Rufaa la
Kangwa itakuwa mkombozi kwa wananchi wa mkoa wa Mara ambao baada ya
kukamilika ujenzi watakuwa wakipata huduma za hospitali ya rufaa katika
mkoa huo tofauti na awali ambapo waanalazika kwenda hadi Bugando mkoani
Mwanza.
‘’
Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli
kwa kufanikisha kutoa kiasi cha zaidi ya bilioni 15 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambao ulisimama kwa muda mrefu kuanzia
mwaka 2011’’ alisema Dkt Mabula.
Amelitaka
shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
Mara kuhakikisha kuchelewa kwa Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo
hilo hakucheleweshi ujenzi wa ujenzi wa mradi wa hospitali hiyo.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula ameitaka Kampuni ya Kiure Engineering ianyojenga jengo
la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa la Mkendo Plaza
kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tano ifikapo
Desemba 30 2019 vinginevyo mkataba wa ujenzi wa jengo hilo utavunjwa
bila kujali kama kampuni hiyo imefikia asilimia ngapi ya ujenzi na
kampuni hiyo itatakiwa kurejesha gharama za ujenzi.
Hatua
ya Dkt Mabula inafuatia kampuni hiyo ya Kiure kushindwa kukamilisha
ujenzi wa jengo hilo tangu kuingia kwa mkataba wa ujenzi mwaka 2015. Kwa
mujibu wa Mhandsi wa ujenzi wa jengo hilo, kampuni ya Kiure iliingia
mkataba wa ujenzi wa jengo hilo mwaka 2015 na ujenzi kuanza rasmi 2017.
0 comments:
Post a Comment