METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 4, 2019

Wimbo wa JAMAFEST2019 Wampa Dili Peter Msechu



*******************
Na Mwandishi Wetu
Wimbo mpya wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msanii Peter Msechu, umeteuliwa kuwa wimbo maalum katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki linalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Septemba 21-28 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za wimbo wa JAMAFEST2019 kuteuliwa kuwa wimbo rasmi wa Tamasha hilo maarufu Afrika Mashariki zilifahamika baada ya Msechu kuandika katika ukurasa wake wa Instagram akimshukuru Mungu kwa wimbo wake huo kupitishwa.
Akiongea baada ya kupigiwa simu kutoa ufafanuzi juu ya kuchaguliwa kwa wake kuwa kuwa maalum katika tamasha la JAMAFEST, Msechu alisema kuwa alitunga wimbo huo baada ya uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwaomba wasanii mbalimbali kutunga wimbo ambao ungetumika kama wimbo maalum wa Tamasha.
“Wasanii tupo wengi sana kwa mimi kupata fursa hii ya kuimba katika ufunguzi tamasha hili kubwa la JAMAFEST kwangu ni heshima kubwa sana. Tulikuwa wasanii wengi tuliotunga nyimbo kwa ajili ya Tamasha lakini wimbo wangu umechaguliwa ni furaha kubwa”, alieleza Msechiu.
Amesema kwa sasa anaandaa video ya wimbo huo ili uweze kutumika kuhamasisha watanzania na watu wa Afrika Mashariki kushiriki katika Tamasha ambalo lengo la kudumisha uridhi wa utamaduni, Sanaa za mikono na ubunifu, biashara na kukuza Akiongea kuhusiana na Wimbo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST, Bi. Joyce Fissoo alisema kuwa mchakato wa uteuzi wa wimbo rasmi kwa ajili ya Tamasha la JAMAFEST haukuwa rahisi kwani kulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na wasanii wengi wakujitokeza na kufanya utunzi wawimbo kwa ajili ya tamasha .
“Mchakato wa kupata wimbo wa Tamasha ulikua mgumu kutokana na wasanii kujitokeza na baada ya kusikiliza nyimbo zote ndipo Sekretarieti ya Maandalizi ya Tamasha inayoundwa na Wajumbe kutoka nchi sita wanachachma wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikauchagua wimbo wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msechu kuwa ndio wimbo wa tamasha”, alieleza Bi. Fissoo.
Tamasha la JAMAFEST ni tamasha lililopitishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuenzi na kulinda utamaduni wa makabila ya Afrika Mashariki. Tamasha hili hufanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi wanachama ambapo mwaka huu tamasha hilo litafanyika nchini Septemba 21-28 katika Uwanja wa Taifa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com