Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 4 Septemba 2019 Jijini Tel Aviv nchini Israel akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 4 Septemba 2019 Jijini Tel Aviv nchini Israel akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima.
Na Mathias Canal, Telaviv-Israel
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) leo tarehe 4 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari.
Katika kikao kazi
hicho kilichofanyika katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Jijini Tel Aviv
nchini Israel, Mhe Hasunga amemualika Bi Sivan kutembelea nchini Tanzania ili
kuwekeza kadhalika kusaidia katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema kuwa kampuni
hiyo inatakiwa kuongeza mshikamano na serikali ya Tanzania ili kuendelea
kutatua sehemu ya matatizo ya wananchi huku kuimarisha mpango wao wa kutoa suluhisho la Israeli na ujuzi kwa wale wanaohitaji
kuishi katika vijiji vya Kiafrika.
Waziri Hasunga amemuhakikishia
Bi Ya’ari kuwa Tanzania ni nchi nzuri katika uwkeezaji na sehemu salama ya
kuishi huku serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli
ikiendeleza juhudi za kuboresha maisha ya watanzania na kuimarisha uchumi wa
nchi.
Hata hivyo ameipongeza kampuni
hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi za Afrika katika sekta ya nishati
ya jua ikiwa ni pamoja na mchango wao katika kutekeleza miradi ya maji safi, na
Kusaidia vituo vya watoto yatima.
Alisema kuwa Tanzania
ni sehemu salama na imara katika uwekezaji, kwani serikali imeanzisha kituo cha
uwekezaji (TIC) ambacho ni Taasisi ya msingi ya serikali yenye jukumu la
kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji.
Tanzania inaongoza kwa uwekezaji
katika Afrika Mashariki na imeweza kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za
Marekani bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda dola za Marekani bilioni 0.7 na
Kenya dola za Marekani bilioni 0.67. “Kutokana na hatua mbalimbali
zinazochukuliwa na Serikali kuvutia uwekezaji nchini, hali ya uwekezaji
imeimarika ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Ripoti mbalimbali za
uwekezaji duniani zinaonesha kuwa Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji
miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki
Taarifa ya Uwekezaji ya
Dunia (World Investment Report) ya mwaka 2018
inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD)
imebainisha kiasi hicho kikubwa cha uwekezaji huku Taarifa nyingine ya“The
Africa Investment Index (AII) 2018” inaonesha kuwa Tanzania
imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 za Afrika katika kutoa fursa za masoko na
vivutio vya uwekezaji.”
Kwa upande wake Mwanzilishi
na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari
akizungumza katika kikao kazi hicho ameridhia ombi la Waziri Hasunga la
kuongeza uwezekano wa kuisaidia Tanzania na kusema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa
tisa atawasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuainisha maeneo ya uwekezaji.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga yupo katika ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel ambapo atakutana
na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo
miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa
kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu
mpya za kilimo nchini Israel.
Pia, Mhe Hasunga atakutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo
mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania
MWISHO
0 comments:
Post a Comment