Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, tarehe 13 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, tarehe 13 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, tarehe 13 Septemba 2019.
Sehemu ya watumsihi wa Wizara ya Kilimo wakifuatilia kikao kazi hicho wakati wa mkutano ulioitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, tarehe 13 Septemba 2019.
Na
Amani Kassimba, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Japeth Hasunga tarehe 13 Septemba 2019 aliwaagiza watumishi wa wizara
yake kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo ili kuongeza uzalishaji wa mazao
nchini.
Amewataka
wataalamu kuzingatia dira ya wizara ili kukifanya kilimo kuwa cha kibiashara na
cha faida kwa wakulima kote nchini.
Waziri
Hasunga ametoa agizo hilo Ijumaa (13.09.2019) wakati alipofanya kikao cha kazi
na wafanyakazi wote wa wizara ya kilimo waliopo makao makuu Jijini Dodoma.
“Lengo
la wizara yetu ni kuhakikisha nchi inazalisha mazao ya kutosha na kuwa na utoshelevu
na usalama wa chakula muda wote” alisema Waziri
Alieleza
katika kikao hicho kuwa uzalishaji wa mazao ya
chakula umewezesha nchi kuwa na utoshelevu asilimia 124 mwaka 2018 na asilimia 119 mwaka 2019.
Waziri
Hasunga aliwataka watumishi wa wizara hiyo kuweka mipango inayotekelezeka
kitaalam ili kujibu hitaji la wakulima nchini ikiwa ni pamoja na elimu ya
kilimo cha kisasa na chenye tija katika eneo dogo.
“Andikeni
miradi ili wizara ipate pesa zaidi za kutekeleza shughuli za uzalishaji mazao
nchini na badala ya kutegemea bajeti ya serikali ili kufikia tija ya
uzalishaji” Waziri Hasunga
Alisema
Tanzania ina hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali lakini
hali ya uzalishaji imeendelea kushuka kila mwaka kutokana na wataalam
kutotimiza majukumu yao.
Ili
kufikia uzalishaji mkubwa na wenye tija amewashauri wataalam wa wizara ya
kilimo kujifunza uzoefu na teknolojia iliofikiwa na nchi za Kenya,Rwanda na
Israel ambazo zimepiga hatua kubwa kuzalisha mazao katika eneo dogo.
“Israel,
Rwanda na Kenya wanafanya vizuri katika uzalishaji,kajifunzeni ili tubadilishe
kilimo chetu kiwe na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la taifa ” alisisitiza
Waziri
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao hicho
aliwasihi wafanyakazi kujituma na kutumia vizuri fedha za umma ili miradi inayotekelezwa na wizara
iwanufaishe wakulima.
Mgumba
aliwataka watumishi hao kuongeza weledi wa ufanyaji kazi ili kupunguza gharama
za uzalishaji na mkulima apate bei nzuri ya mazao yake sokoni.
Naye
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisisitiza suala la matumizi ya Tehama
kuzingatiwa katika kuongeza ufanisi wa kazi za wizara ikiwa ni pamoja na
upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao na utendaji kazi.
Bashe
aliwakumbusha watumishi hao kuwa wizara ya kilimo ndio imeajili watu asilimia
70 hivyo mafanikio ya utekelezaji wa Ilani yakiendelezwa yatasaidia Chama cha
Mapinduzi kuendelea kuungwa mkono na wananchi.
“Uwepo
wa Chama cha Mapinduzi madarakani utaimarika zaidi endapo sekta hii ya kilimo
iliyoajili watanzania wengi itatoa mchango unaokusudiwa katika uchumi”alisema
Naibu Waziri Bashe.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Matherw Mtigumwe alimshukuru na kumhakikishia
Waziri Hasunga kuwa wataalam walio chini yake wataongeza kasi katika ufanyaji
kazi ili wizara ifikie malengo ya nchi.
Wizara
ya kilimo ina watumishi 974 kati yao watumishi 452 wapo makao makuu na wengine
522 wapo kwenye taasisi, vyuo na wakala nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment