METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 29, 2021

WAZIRI JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI NCHINI KUPANDA MITI ISIYOPUNGUA MILIONI 1.5 KILA MWAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Seleman Jafo ameziagiza Halmshauri zote hapa nchini kupanda miti isiyopungua Milioni moja na laki tano kila mwaka kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo husababisha madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa Mazingira


Waziri Jafo ametoa maagizo hayo leo jijini Dodoma wakati zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Medeli lilipo jijini hapa, amesema hivi sasa hali ya hewa imebadilika katika maeneo mbalimbali kutokana na uharibifu wa mazingira huku maeneo mengine yakiwa ni makame.


‘’upandaji huu wa miti unatusaidia sana kuhakikisha tunarekebisha mabadiliko ya tabia ya nchi’’amesema Jafo


Aidha, Waziri Jafo amesema katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wameanzisha kampeni kabambe ya Usafi wa Mazingira na Utunzaji wa Mazingira kukabiliana na mabadiliko hayo.


"kampeni hii ili itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Philip Mpango tarehe 5 ya mwezi wa 6 na tunataka Tanzania iwe nchi ya mfano Duniani kokote mtu akitoka anakuwa anatamani kuja hapa kutokana na Mazingira yaliyopo’’ amesema Jafo


Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema kwenye ajenda kama Mkoa ni kuhakikisha kuwa Mazingira yanakuwa ya kijani.


"Kama viongozi wa Mkoa tutatekeleza maelekezo yatakayotolewa na Ofisi ya makamu wa Rais  Muungano na Mazingira na tuko tayari kwa  jambo hili ambalo limeanzishwa na litatekelezeka’’ amesisitiza Mtaka


Kamishna Mhifadhi Misitu Profesa Dos Santos Silayo ameahidi kushirikiana kwa kuifanikisha kampeni hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kampeni hiyo.


Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Antony Peter Mavunde amesema kutokana na hali ya hewa ya Dodoma inahitaji muamko mkubwa wa upandaji miti huku akiahidi kuwa kampeni hiyo inafanikiwa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.


Hatahivyo, kampeni hiyo ambayo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataizindua June 5 kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani, Waziri jafo aliteua Wajumbe 14 washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi shindani Duniani katika utunzaji wa Mazingira.


CHANZO; DODOMA NEWS

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com