Vijana zaidi ya 500 wilayani
Bagamoyo wanatarajiwa Kunufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Kambi
maalum itakayofanyika mwezi Septemba Katika Kijiji cha mandera Wilayani
Bagamoyo.
Kambi hiyo iliyopewa jina la
“Kambi Moto” inatarajiwa kufanyika kwa siku 10 na itaanza rasmi Septemba
3, mwaka huu na kufunguliwa na Katibu wa UVCCM Taifa, Mwl Raymond
Mwangala ambapo pamoja na Mafunzo ya ujasiriamali, vijana hao
watashiriki Shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi wa Darasa
pamoja na Kuanza Ujenzi wa ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi wilayani
humo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa
Chama cha mapinduzi Uvccm, Mkwayu Makota, amewataka Vijana kuchangamkia
Fursa hiyo kwakua mafunzo hayo yatawaongezea maarifa mengi
yatakayowasadia Kujiajiri.
“Tunawashukuru sana Viongozi wetu
wa ngazi zote Za Vijiji,Madiwani ,Wabunge na Wakurugenzi pamoja na mkuu a
Wilaya kwa namba wanavyotupa Kipaumbele Vijana hasa kwenye Kupigania
Mikopo ya Vijana nasi kama Umoja wa Vijana tumeona ni vyema Tuanzishe
Kambi hii ili kuzidi kuongezeana maarifa ” alisema Mkwayu Makota
0 comments:
Post a Comment