Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 27 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
Serikali
imesema kuwa inaimarisha mikakati yake ili kuwa na uwezekano wa kuwa na
malighafi toshelevu katika viwanda vyote nchini.
Ifahamike
kuwa malighafi nyingi zinazotumika viwandani asilimia kubwa zinatokana na sekta
ya kilimo hivyo moja ya mkakati madhubuti ni kusimamia kwa weledi sekta hiyo
ili kuwa na malighafi nyingi na za kutosha.
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba 2019
wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani
Songwe.
Alisema
kuwa miongoni mwa majukumu muhimu ya Wizara ya kilimo ni kuimarisha Mchango wa
sekta ya kilimo ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji na tija.
"Ni
lazima tuhakikishe kuwa watu wanazalisha kwa ajili ya biashara sio chakula
pekee na gharama wanazotumia ni lazima wahakikishe zinarudi ili waone faida ya
kilimo" Alikaririwa Mhe Hasunga
Waziri
Hasunga ameeleza kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo ina jukumu la
kuhakikisha umasikini unapungua kwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima ili kilimo
kiendelee kuingiza fedha nyingi za kigeni na kuchangia kwa wingi pato la Taifa.
Kadhalika
ametaja Mikakati mingine ya wizara ya kilimo kuwa ni pamoja na Pembejeo
(Mbegu bora, Mbolea, na Viuatilifu) kufika kwa wakati kwa wakulima ambapo
amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kununua mbegu Bora kwani zinaweza
kukinzana na magonjwa na nyingi zinastahimili ukame.
Kuhusu
masoko ya mazao ya wakulima waziri Hasunga amesema kuwa wizara yake imekuja na
mkakati maalumu wa kuanzisha kitengo cha masoko kitakachokuwa na majukumu ya
kubainisha masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima.
"Ni
lazima kufanya biashara kisasa kwa kujua mahitaji ya soko kabla ya kuzalisha
mazao ya kilimo ili wakulima wanapozalisha tayari wawe wanajua watauza wapi
mazao yao" Alisisitiza Mhe Hasunga
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi ambao ni wakazi wa mamlaka ya
mji mdogo wa Vwawa na ameneo ya jirani, Waziri Hasunga amewataka wananchi
kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe
Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha ufanisi wa shughuli za maendeleo
katika Jimbo la Vwawa na Taifa kwa ujumla.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment