
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiweka shada la maua katika
Kaburi la Rubani Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ambaye
alifariki katika ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika
hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara ambaye amezikwa Septemba 26,
2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo na mkewe Tina Mabeyo wakiweka shada la maua katika
kaburi la mtoto wao Rubani Nelson Mabeyo ambaye alifariki katika ajali
ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Mkoani Mara ; ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha
Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (wa pili kushoto) na wakuu wa mikoa ya Mwanza, Mara,
Shinyanga, Kagera, Kigoma na Dar es Salaam wakiweka shada la maua katika
Kaburi la Rubani Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ambaye
alifariki katika ajali ya ndege iliyotokea Septemba 23, 2019 Seronera
katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, ambaye amezikwa
Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani
Simiyu.

Baadhi ya askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania wakiweka Jeneza lenye mwili wa mtoto wa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson
Mabeyo aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani
Mara ; ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanza
wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo na mkewe Tina Mabeyo wakishuhudia jeneza lenye mwili
wa mtoto wao Nelson Mabeyo ambaye alifariki katika ajali ya ndege
Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani
Mara likishushwa kaburini wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Septemba
26, 2019 Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Maaskofu wa Katoliki kutoka
Majimbo ya Mara na Geita wakiweka shada la maua katika kaburi la mtoto
wa Mkuu wa majeshi Jenerali katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti Venance
Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo aliyefariki katika ajali ya
ndege Septemba 23, 2019 Seronera Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba
26, 2019 katika Kijiji cha Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la
Geita akiongoza ibada ya mazishi ya mtoto wa Mkuu wa majeshi Jenerali
Venance Mabeyo, marehemu rubani Nelson Mabeyo aliyefariki katika ajali
ya ndege Septemba 23, 2019 Seronera katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Mkoani Mara, ambaye amezikwa Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha
Masanza wilayani Busega Mkoani Simiyu.
…………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mamia ya wananchi kutoka mikoa ya
Simiyu, Mara, Shinyanga, Mwanza na Dar es Salaam wameshiriki katika
mazishi ya mtoto wa Mkuu wa Majeshi marehemu Nelson Mabeyo aliyekuwa
rubani wa ndege ya Shirika la Auric Air, ambaye alifariki Septemba 23,
2019 kwa ajali ya ndege iliyotokea katika Uwanja mdogo wa Seronera
uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.
Mazishi hayo yamefanyika
Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanzakona wilaya ya Busega Mkoani
Simiyu, ambapo yalitanguliwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yuda Tadei lililipo kijijini hapo ambapo ni
nyumbani kwao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.
Akihubiri wakati wa ibada ya
mazishi, Askofu Michael Msonganzila, Jimbo Katoliki Musoma amewasihi
waombolezaji wote kuendelea kuifariji na kuiombea familia ya Mkuu wa
Majeshi ili wapokee msiba huo kwa jicho la imani, masikio ya imani na
kama mpango wa Mungu.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akitoa salamu za serikali
amesema “marehemu Nelson Mabeyo alikuwa kijana mcheshi na mchapakazi
leo hatuko naye tena nitoe pole kwa familia ya Jenerali Mabeyo, sisi ni
wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea niwaombe tuendelee kuwaombea katika
kipindi hiki kigumu Mwenyezi Mungu awape ustahimilivu.”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Simiyu
na wakuu wa mikoa ametoa pole kwa familia ya Mkuu wa Majeshi na
kumshukuru kwa namna Mkuu alivyowaunganisha watu wa Masanza, Busega na
Simiyu katika masuala mbalimbali ya ikiwemo Ujenzi wa Kanisa ambalo
ibada ya mazishi ya marehemu Nelson imefanyika.
Kwa upande wake Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenrali Venance Mabeyo amewashukuru watu wote
walioshirikiana na familia yake tangu msiba wa mwanaye Nelson ulipotokea
, ambapo amesema kama familia hawauchukulii msiba huo kama adhabu bali
makusudi ya Mungu mwenyewe kwa mtoto wao .
Mazishi ya marehemu Nelson
Mabeyo yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,
viongozi na Maafisa wa JWTZ walioko kazini na wastaafu, mawaziri na
manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa Taasisi, viongozi wa Vyombo vya
Usalama, wabunge, Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Kagera,
Kigoma, Mwanza na Dar es salaam , kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa
Simiyu na wakuu wa wilaya.
0 comments:
Post a Comment