Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia sukari, alipotembelea kiwanda
cha Kilombero Sugar, kilichopo katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,
Septemba 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia maelezo ya uzalishaji wa sukari,
wakati alipotembelea kiwanda cha Kilombero Sugar, kilichopo katika Wilaya ya
Kilombero, mkoani Morogoro, Septemba 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, katika kiwanda cha
Kilombero Sugar, kilichopo katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,
Septemba 17.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipanda mti baada ya kuweka jiwe la msingi
la kituo cha afya cha Malolo, wilayani Kilosa Morogoro, Septemba 17.2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassimu Majaliwa amesema
hajaridhishwa na gawio la sh milioni 800 linatolewa na kiwanda cha Sukari cha
Kilombero ambacho uzalishaji wake ni kikubwa ikilinganishwa na kiwanda cha
sukari cha Moshi TPC ambacho kinatoa gawio la sh. billion 15 kwa mwaka.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati alipotembelea kiwanda hicho, akiwa katika
siku ya nne ya ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro. Amevitaka viwanda vya
sukari nchini kuzaliza sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji.
Akizungumzia kuhusu vibali vya uagizaji
wa sukari, Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kutoa nafasi ya kuagiza sukari
kwa wenye viwanda ili kuepuka ujanja uliokuwa ukifanywa na baadhi ya
wafanyabiashara ambao walikuwa wakiagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo
nyingine ilikuwa haina ubora.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema
Tanzania bado kuna uhitaji mkubwa wa sukari hususani ya viwandani, hivyo
kusababisha Serikali kutoa vibali kwa wamiliki wa viwanda kuagiza sukari kutoka
nje ya nchi. “Viwanda vya ndani vya sukari vihakikishe vinaongeza uzalishaji wa
sukari ya viwandani ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Kilimo, Omary Mgumba amesema mahitaji ya sukari kwa mwaka huu nchini
yameongezeka hadi kufikia tani 710,000 ikilinganishwa na tani 610,000 za mwaka
jana.
Amesema ongezeko hilo limechangiwa na
kuongezeka kwa viwanda vipya vinavyotumia sukari ya viwandani, ambapo kwa sasa
mahitaji ya sukari ya viwandani yamefikia tani 165,000.
Amesema mahitaji ya sukari za majumbani
kwa sasa ni tani 545,000, ambapo kiwanda cha Kilombero kinazalisha tani
134,000, kiwanda cha Manyara tani 6,000, kiwanda cha Mtibwa tani 39,000 na TPC
cha Moshi tani 100,000.
Naibu Waziri huyo amesema ili
kukabiliana na upungufu wa sukari Serikali imeweka mkakati wa kuanzishwa kwa
viwanda vipya vya sukari vya Bagamoro ambacho kitaanza kuingiza awamu ya kwanza
ya sukari sokoni tani 35,000 ifikapo mwaka 2022 na kiwanda cha Mkulazi
kinatarajiwa kuzalisha tani 200,000 na cha Mbigili tani 50,000.
Akitoa taarifa za kiwanda hicho
Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Balozi Amry amesema Kampuni ya Sukari ya Kilombero
imezingatia kikamilifu wito wa Serikali wa kukuza uzalishaji na kuweka mipango
thabiti ya upanuzi wa uzalishaji wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kusindika miwa.
Mradi huo utagharimu sh. bilioni 700.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa muda wa wiki mbili
kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa awe amechimba visima katika
kata ya Ruaha kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa eneo hilo kupata maji safi na
salama.
Ameyasema hayo baada ya wakazi wa kata hiyo kusimamisha msafara
alipokuwa akielekea kata ya Malolo. Amesema halmashauri hiyo inakusanya zaidi
ya sh. bilioni mbili kwa mwaka hivyo inatakiwa kutenga kiasi cha fedha za
mapato kugharamia miradi ya maendeleo ya wananchi.
Waziri Mkuu amesemaSerikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt.
John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, ambayo inalenga kuwaondolea
wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa kuhakikisha
huduma hiyo inapatikana karibu na maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment