METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 17, 2019

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AENDELEA KUWASHA UMEME VIJIJINI


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika Kijiji cha Mlamleni wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwasili katika Kijiji cha Mlamleni ili kuwasha umeme. Wa Pili kulia ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa vitongoji vya Kisasa na Churwi mara baada ya kufika katika Vitongoji hivyo kukagua kazi ya usambazaji umeme.

Na Hafsa Omar, Pwani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ameendelea kukagua utekelezaji wa kazi ya kusambaza umeme vijijini pamoja na  kuwasha umeme katika vijiji mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo mwaka 2021.

Tarehe 16 Septemba, 2019, alikagua kazi ya usambazaji umeme katika vitongoji vya Kisasa na Churwi pamoja na kuwasha umeme katika kijiji cha Mlamleni  Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mlamleni,  Naibu Waziri alieleza kuwa wakandarasi wakikamilisha miradi ya umeme na kukabidhi kwa  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wananchi wataunganishiwa kwa bei ile ile ya shilingi 27,000.

Aliwaahidi wananchi wa kijiji hicho kuwa, umeme utasambazwa kwa wananchi wote kwani Tanesco inahitaji wateja ili Shirika hilo liweze kujiendesha lenyewe, hivyo ni lazima wateja wengi wapatikane.

Naibu waziri alisema kuwa, Wilaya ya Mkuranga ni moja ya wilaya ambazo zipo kwenye mradi wa umeme wa ujazilizi awamu ya pili (A) utakaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo maeneo mengi zaidi yataunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000.

Vilevile, alisema kuwa, wilaya hiyo itasambaziwa umeme kupitia mradi wa Peri-Urban ambapo wananchi 4293 ambao ni wateja wa awali wataunganishwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com