Watendaji wa chama hakuna kulala
Na Mwandishi wetu, Morogoro
Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Morogoro
kimejianda vyema na kusema kipo tayari kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa,
Vijiji na Vitongoji kwani ndio kitovu cha kushika hatamu za utawala wa dola
hivyo kitaheshimu sheria na matakwa ya demokrasia.
Kimesema Uchaguzi huo licha ya kuwa ni muhimu
na kipimo cha kuaminiwa kwa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu
mwaka 2020,CCM na serikali zake hakina sababu za kushindwa .
Hayo yameelezwa jana na Katibu wa CCM mkoa
Morogoro Shaka Hamdu Shaka wakati akitoa tathimini ya zoezi la uchukuaji fomu
za kuomba kuteuliwa na chama kugombea nafasi ya vitongoji alipokuwa akizungumza
na viongozi wa kata, matawi na mashina morogoro mjini na kuwataka
kuendelea kujipanga, kufuata, kanuni, taratibu za kisheria na kikatiba zilizowekwa
na Serikali.
Shaka alisema kila kiongozi wa CCM ana wajibu
wa msingi kuhakikisha chama kinapitisha wagombea wenye weledi na sifa,
wanaokubalika kwenye jamii na watakaokuwa tayari kuwatumikia wananchi.
Alisema wakati uchaguzi huo ukifanyika Novemba
mwaka huu, serikali za CCM zimejitahidi vya kutosha kuimarisha huduma za
kiwajibu kwa jamii, kuinua uchumi na kushughulikia kero sugu na
kuzitatua.
"Nawapongeza sana makatibu wa wilaya,
kata na matawi hamasa na mwitikio kwa wanaccm umekuwa mkubwa katika kuchukua
fomu za vitongoji ndani ya chama tunaendelea kusisitizana kuwa Uchaguzi huu ni muhimu
kwa mustakabali wa chama. Mtendaji yeyote wa chama atakayezembea
atahesabiwa ni msaliti na amekihujumu chama. Usaliti na hujuma si sifa njema
bali dhambi isiosameheka" Alisema shaka
Aidha amewakumbusha watendaji hao wa chama
muda wote kuzingatia maelekezo ya kikanuni na kisheria kuhusu usimamizi na
kufuata taratibu, miongozo na kanuni za chama na Serikali ili kutimiza dhana ya
demokrasia kivitendo.
"Viongozi wa kata, matawi chama na
jumuiya sambamba na viongozi wa chama ngazi za vijiji, mitaa na vitongoji
lazima msimame pamoja zisimame pamoja na mfanye kazi usiku na mchana bila
kuchoka wote kwa umoja wenu na mshikamano mjitume kama wafanyavyo siafu ili
tushinde vizuri ili kulinda heshima ya Rais Magufuli mbele ya macho ya
dunia" Alisisitiza Shaka .
Alisema CCM inajua kina sifa za kushinda
kwakuwa siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuheshimu na kufuata taratibu lakini
mahasimu wao kisiasa alidai wanajiandaa kwa ulalamishi na uzushi wa kutengeneza
baada kupotezea muelekee na kupoteza dira kisiasa.
Katibu huyo aliwaeleza watendaji wake kazi na
dhamana ya kuwatumikia wananachi kimepewa CCM hivyo kuwaachia wengine hatua
hiyo itahesabika ni makosa kisiasa kiufundi na kihistoria
"Tunashiriki uchaguzi kwa kujiamini
tutashinda kwa haki usawa na amani. CCM mkoa wa morogoro Tunaahidi kufuata
taratibu zote za kikanuni na kikatiba. Tutakaposhindwa tutaheshimu matokeo na
wenzetu pia wawe waungwana wa kutii matakwa na uamuzi wa
wananchi "Alisema Shaka
Source Majira, mtanzania
0 comments:
Post a Comment