Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na
Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akiongozana na Mkuu
wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri,alipowasili kwa ajili ya
kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika
katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
Mhe.Jabir Shekimweri,akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya
Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa anayefatia ni Afisa mifugo Mkuu
Idara ya malisho na Rasilimali ya vyakula vya mifugo Israel Kilonzo
alipowasili kwa ajili ya kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa
malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
Mhe.Jabir Shekimweri,akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kwa ajili ya
kufungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika
katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa wa
malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa
Mhe.Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kufungua Kikao cha mafunzo
rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali na wadau wa
malisho nchini yaliyofanyika leo kushoto ni Mkurugenzi wa
Utafiti,Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa na
upande wa kulia ni Mkuu wa Kampasi Lita Mpwapwa yaliyofanyika katika
chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti ,Mafunzo
na Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akifafanua jambo
kwa washiriki wa mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba
ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha
Mifugo Lita Mpwapwa.
Meneja wa shamba la kuzalisha
malisho na mbegu za malisho Vikuge Kibaha Ricahard Mdegipala,akitoa
taarifa katika kikao cha mafunzo rejea kwa wataalam wa malisho kutoka
mashamba ya Serikali na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika
chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Sehemu ya washiriki kutoka
sehemu mbalimbali wakifatilia ufunguzi wa mafunzo ya wataalamu na wadau
wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Afisa Mifugo na Mtaalam wa
malisho kutoka Mabuki Bi.Asteria Mwaya,akitoa taarifa wakati semina ya
mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika
chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya
Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa,akisisitiza jambo kwa wataalamu na
wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita
Mpwapwa.
Meneja wa Shamba la malisho
Langwira Mbarali mkoani Mbeya ,akitoa taarifa wakati semina ya mafunzo
ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha
Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,mafunzo na
Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Angello Mwillawa,akizungumza jambo na
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri mara baada ya semina ya
mafunzo ya wataalamu na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika
chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na
Ugani kutoka wizara ya Mifugo Dkt.Mwillawa akitoa maada katika kikao
cha mafunzo ya rejea kwa wataalam wa malisho kutoka mashamba ya Serikali
na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita
Mpwapwa.
Sehemu ya wataalam kutoka sehemu
mbalimbali wakiendelea kuchangia mada katika semina ya mafunzo ya
wataalam na wadau wa malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo
Lita Mpwapwa.
……………….
Na.Alex Sonna,Mpwapwa
Wataalamu wa malisho kutoka halmashauri mbalimbali
hapa nchini, wametakiwa kutoa elimu hiyo kwa wafugaji ili kuwajengea
uwezo wa kutambua matumizi bora na endelevu ya nyanda za malisho.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Mhe. Jabir Shekimweri wakati akifungua mafunzo ya wataalamu na wadau wa
malisho nchini yaliyofanyika katika chuo cha Mifugo Lita Mpwapwa.
Mkuu wa Wilaya Shekimwer alisema elimu ya utunzaji
malisho ni muhimu kwa wafugaji kwa sababu itawasaidia kujua nini
wanatakiwa kufanya ili kudhibiti uhaba wa malisho pale unapotokea.
Alisema lengo lao ni kuona maafisa ugani hao
wanatumia nafasi walionayo kutoa elimu hiyo kiufanisi kwa wafugaji
katika halmashauri mbalimbali wanazotoka ambayo itasaidia kupunguza
migogoro baina ya wafugaji na wakulima kugombea maeneo ya malisho.
“Mafunzo mliyoyapata mkayatoe kwa wafugaji katika
sehemu mnazotoka tumieni nafasi yenu ili kuisaidia serikali ya awamu ya
tano kuboresha sekta ya Mifugo,” amesema Shekimwer.
“Mnapaswa kuhamasisha na kuongeza uvunaji wa
malisho na matumizi ya teknolojia rahisi za kukata,kufunga,na kuhifadhi
majani na masalia ya mazao ili yatumike wakati wa uhaba” alisema
Alisema kuwa hayo yakitekelezwa anaimani itasaidia
wafugaji kujenga Utamaduni wa kusindika masalia ya nafaka na kuchakata
kwa ajili ya kulisha Mifugo yao.
Pia ameiopongeza wizara ya Mifugo kutokana na kuwa
mstari wa mbele kutoa mafunzo kwa maafisa ugani mara kwa mara ambayo
yanasaidia kuwakumbusha majukumu yao ya kazi.
Aidha alisema kuwa serikali ya awamu ya tano
inalenga kuboresha sekta hivyo,hivyo ni vema maafisa ugani na wataalamu
wa malisho kuzingatia elimu wanayopewa ili nao wakaitoe kwa wafugaji.
Awali akieleza lengo la semina
hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara hiyo,Dkt.Angello
Mwillawa, alisema ili kukabiliana na changamoto pamoja na migogoro
inayowakumba wakulima na wafugaji, wizara umeona iwakutanishe wataalam
wa malisho nchi nzima ili kila mmoja aainishe changamoto anazokutana
nazo katika eneo lake.
Dkt.Mwillawa aliwataka wataalam
hao kuwa wa wazi kueleza changamoto zilizopo ili wizara iweze kufahamu
wapi pa kuanzia katika kutatua changamoto na migogoro hiyo.
Akizungumzia changamoto ya
upatikanaji wa mbegu za malisho ambayo ilielezwa na washiriki, alisema
hakuna changamoto kama hiyo mbegu zipo nyingi tatizo ni uzembe wa
wataalam hao katika kuagiza na kufuatilia kwa karibu ili ziwafikie
katika vituo vyao.
Mkurugenzi huyo aliwataka
kuhakikisha wanakuwa ‘na mtandao bora na kubadilishana uzoefu baina ya
eneo moja na jingine jambo ambalo litawapa wepesi katika kutatua kila
changamoto.
Pia aliwataka kuongeza thamani
katika bidhaa zao ‘na kuainisha aina ya mbegu wanazozalisha na kuuza kwa
wafugaji pamoja na faida au hasara yake hiyo itakuwa rahisi kufanya
biashara.
Kwa upande wao washiriki wa
semina hiyo waliishukuru wizara kwa kuandaa warsha hiyo huku wakieleza
changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo uwezo mdogo wa kuendeleza
maeneo yao hivyo kujikuta maeneo mengi yakubali kuwa vichaka licha ya
kuwa na uhitaji wa maeneo.
Akizungumza Meneja wa Shamba la
Malisho Vikuge wilayani kibaha mkoani Pwani, Richard Mdegipala, alisema
wao wana eneo la ukubwa wa hekta 515 lakini hekta 215 ya shamba au eneo
hilo ni pori wameshindwa kuliendeleza wakiiomba serikali iwasaidie.
Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo
ya Mifugo(LITA) Mpwapwa, Moses Mlahagwa, aliwataka wataalam hao
kuhakikisha wanatafuta alama ya kuiweka watakaporejea katika vituo vyao
vya kazi mara baada ya warsha hiyo ili kuonyesha kuwa ilikuwa na tija
kubwa wao.
“Hapo mlipo mtambue kuwa mmebeba
dhamana ya mifugo ya Taifa nanyi ndio mnaotarajiwa kubadili changamoto
za wafugaji kuwa fulsa, jambo la muhimu kwenu mnalotakiwa kulifanyia
kazi ni alama gani mnakwenda ukiacha,”alisema.
Nice my young bro peternchimbi
ReplyDelete