Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000
kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa
aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika
Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa
mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019. Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya
hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa
akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu,
Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella
Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na
Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga.
Askari Mwambenga akiwa amemkanyaga nyoka huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Nyoka akiuawa na baada ya kuuawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment