

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya,
Dkt Dorothy Gwajima, akizungumza wakati wa kufunga mkutano
uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta
ya Elimu alipokuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph
Nyamhanga

Sehemu ya wadau wakifatilia kwa
umakini Hotuba ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy
Gwajima,wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya
tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa akimuwakilisha
Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya,
Dkt Dorothy Gwajima,akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano
uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta
ya Elimu alipokuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph
Nyamhanga jijini Dodoma.

Wadau wakimsikiliza kwa umakini
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima (hayupo
pichani) wakati wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu
kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu alipokuwa
akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga jijini
Dodoma.

Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro
Bi.Paulina Mbena akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI)
anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima,baada ya kufunga mkutano
uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta
ya Elimu alipokuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph
Nyamhanga jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe,akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya kufungwa kwa mkutano uliowakutanisha wadau wa
elimu kufanya tathmini ya malengo katika sekta ya Elimu uliofanyika
jijini Dodoma kwa siku tatu.
……………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
duniani(UNICEF) wamejipanga kuanzisha mafunzo maalumu kuwapa ujuzi na
kuwakomboa vijana walio nje ya mfumo wa elimu ili nao wanufaike na
mpango wa kupata stadi maisha za kuweza kujiajiri.
Hayo yamebainishwa na
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa,(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima, alipokuwa
akimuwakilisha Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati
wa kufunga mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu kufanya tathmini ya
malengo katika sekta ya Elimu.
Amesema wamejipanga
kuhakikisha wanaanzisha mafunzo hayo kupitia IPOSA, mafunzo hayo ambayo
yatawawezesha vijana walio nje ya mfumo wa elimu kupata mafunzo ya stadi
za maisha na kupata ujuzi na kujiajili na kukuza sekta ya viwanda
vidogovidogo.
“Sisi kama serikali kwa
kushirikana na wenzetu wa UNCEF kupitia kwa IPOSA, tunawapa mafunzo
vijana walio nje ya mfumo, ambao hawakuweza kupata elimu na mafunzo hayo
yatawawezesha kupata stadi za maisha” amesema Dkt Dorothy.
Mbali na hapo ameshauli
elimu ya ufundi ianzie kwenye elimu ya awali na msingi ili kuwawezesha
watoto kukua wakijua namna ya kuunda kitu na kujenga dhana ya stadi za
maisha.
“Elimu ya ufundi
inatakiwa kuanzia kwa watoto katika shule za awali na msingi ili watoto
hawa wanapokuwa wanakuwa na ujuzi na wanakuwa na uwezo wa kuunda kitu au
dhana ya kitu, tofauti na sasa elimu hiyo inatolewa kwa watu wazima
tunakuwa tumechelewa” amesema.
Aidha amesema kama
tunataka kutoka hapa tulipo na kufikia malengo ya nchi ya ifikapo 2025
tufikie uchumi wa Kati, ni lazima tushikilie elimu kwani ndio Jeshi na
msingi wa hayo yote.
Amesema wao kama
serikali wanajitahidi kuhusianisha kati ya elimu na Jamii ili elimu hiyo
iwasaidie katika kujikwamua kupitia nyanja mbalimbali katika kutoka
hapo walipo na kwenda sehemu nyingine kiuchumi kupitia elimu hiyo.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe,
amesema mkutano Kama huo hufanyika kila mwaka na kuna fedha ambayo
hutengwa na Serikali, na washirika wengine wa maendeleo na katika
mikutano kama hii hutumika kufanya tathmini ya kupitia maazimio
waliojiwekea.
Pamoja na kuona
utekelezaji wa maazimio hayo na kushirikisha changamoto zilizopo katika
kutekeleza maazimio waliojiwekea katika kuhakikisha wana toa elimu
iliyobora hapa nchini.
Pia wamekuwa na mijadala
mbalimbali na katika mijadala hiyo, pia wadau wameibua suala la
kuhakikisha katika mipango ya ujenzi wa vyuo na turudi katika falsafa ya
kwamba Kama chuo kimeanzishwa kwa ajiri na Uvuvi kweli kijikite katika
Uvuvi na kuleta tija katika sekta hiyo ya uvuvi.
0 comments:
Post a Comment