
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph
Sokoine (katikati) akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Sera na
Mipango wa Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT).
Kikao hicho kimejadili uratibu wa masuala ya Muungano ikiwa ni pamoja na
upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila Wizara na kimefanyika katika
Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la Bima ya Afya Jijini Dodoma. Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano Bw. Sifuni Msangi na Bi. Lupi
Mwaikambo Mkurugeni Msaidizi Idara ya Muungano.

Bi. Mariam Silim Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Bw. Ezekiel
Chundu Mchumi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi)
wakifuatilia maelezo ya Naibu Katibu Mkuu (hayupo pichani) katika Kikao
cha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Tanzania Bara. Kikao hicho
kimefanyika hii leo Jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika hii leo Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment