Waziri wa Madini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara, watoa huduma na uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita (GGM) mjini Geita.

Sehemu ya Washiriki wa mkutano baina ya wafanya biashara, watoa huduma na Uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita (GGM) mjini Geita.

Waziri wa Madini akiagana na Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mha. Robert Gabriel baada ya kufungua mkutano wa
wafanya biashara, watoa huduma na uongozi wa Mgodi wa Dhabau wa Geita
(GGM) mjini Geita.
Na Issa Mtuwa – Geita
Pamoja na kuupongeza Mgodi wa
Dhahabu wa Geita (GGM) katika masuala ya ulipaji kodi, utekelezaji wa
miradi ya maendeleo kwa jamii (CSR) na kuwa mgodi namba moja nchini kwa
utekelezaji wa Sheria za Madini, bado serikali hairidhishwi na namna
mgodi huo na mingine inavyowashirikisha wananchi moja kwa moja.
Kauli hiyo ilitolewa Septemba 16
na Waziri wa Madini Doto Biteko mjini Geita kwenye mkutano
uliowakutanisha wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali mkoani Geita,
wananchi na uongozi wa GGM. Mkutano huo uliokuwa na lengo la
kufahamishana fursa za kibiashara na utoaji huduma zilizopo kwenye
mgodi wa GGM.
“Naomba niwe mkweli, mgodi wa GGM
ni wakwanza hapa nchini katika ulipaji wa kodi, utekelezaji wa miradi
ya maendeleo ya jamii (CSR) lakini sijaridhishwa na namna ambavyo mgodi
unavyo washirikisha wananchi moja kwa moja ili waone umaana wa uwepo wa
raslimali hii katika mazingira yao,” alisema Biteko.
Aliongeza kuwa, ni wajibu wa GGM
kuwaeleza wananchi fursa zilizopo na namna mgodi unavyowashirikisha ili
madini yanapokwisha wananchi wabaki na kumbukumbu ya uwepo wa dhahabu
hapa mkoani humo.
Pia, Waziri Biteko alitaka baada
ya mkutano huo kuwe na maazimio yatakayo ratibiwa na kusimamiwa na Mkuu
wa Mkoa huku akisisitiza maazimio hayo kueleza namna mgodi huo
unavyokwenda mkieleza namna mnavyokwenda kuwahusisha wananchi.
Kwa upande mwingine, Waziri Biteko
amekemea vikali vitendo vya udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu
wanaopewa fursa ya kufanya biashara na migodi na kueleza kwamba, amekuwa
akipokea malalmiko ya udanganyifu na wizi kwenye migodi unaofanywa na
baadhi ya wasio wema na amewataka kubadilika na kutenda haki ili
kuongeza imani ya kuendelea kuwatumia watoa huduma wa ndani.
Waziri Biteko alisema kuanzia sasa
Kamishna Msaidizi anaye shugulikia masuala ya Ushiriki wa Nchi na
Wananchi katika Sekta ya Madini (Local Content) kutoka ofisi ya Kamishna wa Madini atakuwa anapita kukagua namna utekelezaji wa masuala ya Local content yanavyo tekelezwa na hii sio kwa mgodi wa GGM peke yake bali kwa migodi yote hapa nchini.
Pamoja na kuelezwa kuwa mpaka sasa
mgodi wa GGM una asilimia 97 ya wafanyakazi ni wazawa, bado haitakuwa
na maana kama maamuzi ya mambo mbalimbali yatakuwa yanasubiri asilimia 3
ya wafanyakazi wanaotoka nje.
Halikadhalika, Waziri Biteko
aliwakumbusha watendaji wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake zote
kuhusu agizo alilolitoa akiwa ziarani Mkoani Lindi wiki mbili zilizopita
kuendelea kufuatilia yanayojiri kwenye ziara zake hususani viongozi
kwani patafika mahali wananchi na wadau watatakiwa kupatiwa majibu ya
papohapo ili kuondokana na kero bila kusubiri muda mrefu. Hivyo,
alimtaka kila mtendaji kuwa tayari kupokea simu pindi atakapo muhitaji
na kutolea majibu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema bado kwenye mgodi wa GGM kuna
“figisu figisu” katika kuwapatia ajira wana Geita kwa visingizo
mbalimbali na hususan ujuzi wa lugha ya Kiingereza na kuwataka
kubadilika katika hilo.
“Kuna figisu figisu ya utoaji wa
ajira pale mgodini, moja ya sababu mnasema lugha, hicho Kiingereza sio
ndio kinachofanya kazi, hiyo lugha sioni ulazima wake na sio wakati wote
watakuwa wanaongea muda mwingi ni wakufanya kazi wakiwa wenyewe hata
kisukuma watakuwa wanaimizana kufanya kazi,” alisema Mhandisi Gabrile.
Naye. Meneja Mkuu wa Mgodi wa GGM
Richard Jordinson alisema kama mgodi wamedhamiria kuifanya jamii ya
Geita kuwa sehemu ya mgodi na ndiyo sababu tayari wamewisha sainishana
mikataba mbalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Na kuongeza, ni dhamira yao kuiona Geita yenye dhahabu inakuwa na nuru ya dhahabu na wako tayari kushirikiana na jamii na serikali, kutii mamlaka za serikali na kufuata marekebisho yote yaliyofanywa kwenye sheria ya madini na ndio maana wameamua kukutana na wadau ili wajadili masuala yote.
Na kuongeza, ni dhamira yao kuiona Geita yenye dhahabu inakuwa na nuru ya dhahabu na wako tayari kushirikiana na jamii na serikali, kutii mamlaka za serikali na kufuata marekebisho yote yaliyofanywa kwenye sheria ya madini na ndio maana wameamua kukutana na wadau ili wajadili masuala yote.
Aidha, Uongozi wa GGM umemshukuru
Waziri Biteko na wafanyakazi wote wa wizara kwa ushirikiano wanao upata
mara kwa mara kwani wanaifanya kazi yao kuwa rahisi, mara zote wamekuwa
wakijadiliana na kukubaliana katika masuala mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Anglo Gold Ashanti Bara la Afrika, Sicelo Ntuli alisema mgodi GGM
mwaka 2018 ulitenga bilioni 9.2 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa
mkoa wa Geita peke yake na wanatarajia kuanza kutekeleza miradi hiyo
mwaka wa fedha wa 2019/20.
0 comments:
Post a Comment