Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma jana tarehe 18 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma jana tarehe 18 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa mkutano wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma jana tarehe 18 Septemba 2019.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa
Mbolea Tanzania (TFRA) kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati na bei nafuu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema
hayo jana tarehe 18 Septemba 2019 wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji
wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma.
Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Kilimo imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti uwepo wa
pembejeo feki nchini.
Alisema Kwa upande wa mbolea, tayari Wizara ya
Kilimo imetoa mafunzo na kuwapitisha Wakaguzi 50 wa mbolea ambao wanaenda
kuongeza nguvu kwa kufanya kazi nchi nzima za kudhibiti ubora wa mbolea.
Mhe Hasunga alisema kuwa kwa upande wa
Viuatilifu, ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa
Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na
kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.
Aidha, tayari Wizara imeridhia na kuwapitisha
Wakaguzi (Inspectors) 45 wa kukagua viuatilifu ambao nao wanaenda kuongeza
nguvu nchi nzima kuhakikisha tatizo la viuatilifu feki linamalizika.
Kadhalika Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kudhibiti na kuondokana na changamoto ya
uwepo wa pembejeo ambazo hazikidhi viwango.
Katika mkutano huo Mhe hasunga ameupongeza
uongozi wa TADCOs kwa mwanzo mzuri wa kiuongozi hususani kuwasomea wananchama
wao mapato na matumizi hukuakitoa rai kwa Viongozi wote, kuhakikisha wanaendesha
chama hicho kwa ufanisi mkubwa, uwazi na uwajibikaji kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu za ushirika nchini.
Aliongeza kuwa ana matarajio kwamba, kuanzishwa
kwa chama hicho cha Ushirika kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto
zilizokuwepo na kusaidia kuwanufaisha wakulima kwa kuagiza na kusambaza pembejeo zenye ubora, kwa wakati na bei
nafuu.
“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwakomboa
wakulima nchini kwa kuhakikisha wanazalisha mazao yao kwa tija ili waweze
kuinua hali zao za maisha na kuchangia uchumi wa nchi. Ni ukweli usiopingika kuwa azima hii hawezi
kufikiwa kama wakulima hawatapata pembejeo zenye ubora, kwa wakati na kwa bei
nafuu” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa
“Dhamana mliyonayo ni kubwa sana, hivyo ni matarajio yangu kuwa
mtatimiza jukumu lenu kuu la kuhakikisha mnasimamia usambazaji wa pembejeo za
kilimo wakulima wa Tanzania walio wanyonge kwa uaminifu na uweledi mkubwa.”
Aliwataka (TADCOs) kufuata Sheria, kanuni na taratibu
zote zinazohusu uendeshaji wa biashara ya pembejeo nchini na kuzingatia kanuni
za ushirika. Aidha, kushirikiana na Taasisi
zote zinazodhibiti na kusimamia tasnia ya pembejeo na ushirika nchini kama vile
TFRA, TPRI, ASA, TOSCI, TCDC na TFC ili waweze kuwasaidia wakulima kupata
pembejeo zenye ubora.
Ili kupunguza gharama na kuhakikisha wakulima
wanapata pembejeo sahihi, kwa wakati na bei nafuu, Mhe Hasunga aliwaagiza
Viongozi wenu wa TADCOs kusimamia vilivyo zoezi la uagizaji wa pembejeo kwa
pamoja, moja kwa moja kutoka viwandani na si kwa wauzaji wa kati.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment