
Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye
Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la
mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).

Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu),
Mhe. Stella Ikupa, Akikabidhi baiskeli ya watu wenye mahitaji maalum kwa Bw.
Martine Vicent Mkazi wa Wilaya ya Kigamboni mara baada ya kumaliza kutembelea
mabanda katika Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).

Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye
Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akizungumza na Waandishi Wa Habari (hawapo pichani) Mara baada ya kutenmbelea mabanda katika Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-Maelezo).
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).
Eric Msuya – MAELEZO, Dar es Salaam
26.09.2019
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa amelipongeza Tamasha la Utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(JAMAFEST) kwa kuwazingatiaa watu wote wenye mahitaji Maalumu kwa kuwapa
kipaumbele katika Tamasha hilo.
Ameseyasema hayo leo, mbele ya
Waandishi wa Habari, mara ya baada ya kutembelea Mabanda na kujionea
ubufunifu mbalimbali ya maonyesho ya Tamasha la JAMAFEST, linaloendelea
kufanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Amewapongeza Waandaji wa Tamasha
la JAMAFEST kwa kuwapa kipaumbele watu wenye Ulemavu katika kuwapatia
mabanda, kwa ajili ya kuuza na kuonyesha bidhaa zao katika Tamasha hilo
na kuweza kutangaza biashara zao
“Nitoe Pongezi kwa Waandaji wa
Tamasha hili la JAMAFEST, Muitikio wa watu umekuwa mkubwa hasa kwa kundi
la watu wenye ulemavu, nimejionea vitu vingi vinavyotengenezwa na
walemavu, bidhaa zao ni nzuri kabisa na zipo kwa viwango vya juu sana”
Alisema Mhe. Stella Ikupa
Sambamba na hilo Mhe Ikupa
Amewataka Watanzania kufika katika Viwanja vya Taifa kujionea bidhaa
mbalimbali za kiutamaduni zinazo tengezwa na Watanzania ili waweze kujua
Utamaduni wa Watanzania na Wanaafrika Masharikikwa ujumla.
Pia Mhe. Ikupa amewasisistiza
Watanzania kutumia muda wao mwingi kujionea mambo mbalimbali ya
Utamaduni yanayo fanyika katika Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST
“Ukifika kwenye Tamasha hili la
JAMAFEST hautajuta kupoteza huo muda wako, ila utakuwa umepata kitu
kikubwa cha kujifunza juu ya Utamaduni wa Muafrika” Alisema Mhe. Stella
Ikupa
Aidha katika Ziara hiyo Mhe. Ikupa
amewakabidhi baiskeli za watu wenye mahitaji maalum ndugu Martini
Vicente mkazi wa Kigamboni na Ndugu Rajabu Ismail mkazi wa Magomeni-
Mwembe Chai ambao wote ni Walemavu wa Miguu.
0 comments:
Post a Comment