Oleiboni Mtayani Simanga wa kijiji
cha Kidui, kata ya Kilangali wilaya ya Wilaya ya Kilosa Leo amesimikwa
rasmi kuwa Chief wa kimasai wa ukanda wa mikoa ya Morogoro, Iringa,
Njombe, Mbeya, Songwe na Dodoma.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na
wazee wa kimila kutoka mikoa yote sita kikanda, viongozi wa dini,
viongozi wa serikali, wananchi mbali mbali pamoja na viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi akiwemo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ndugu
Ruta Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, katibu, Katibu
Mwenezi wa CCM Antony Muhando pamoja na viongozi kadhaa wa Chama na
jumuiya.
Akitoa Salam za Chama Katibu wa CCM mkoa aligusia baadhi ya maeneo:
“Mila na tamaduni zetu ifike pahala sasa iwe ni sehemu ya kushamirisha maendeleo katika maeneo yetu” Shaka Hamdu Shaka
“Chief mpya ameainisha hapa kuwa
atasimama upatikanaji wa elimu, kushirikiana na serikali katika
kuhakikisha huduma za kijamii zinaimarika, kuhakikisha mnakuwa na maisha
mazuri pamoja na nyumba za kisasa za kusihi” Shaka Hamdu Shaka
“Nchi yetu inabaraka toka enzi na
asili wingi wa makabila yetu sio chochote kwetu umoja wetu na mshikamano
tuliona ndio msingi wa Taifa letu mwisho wa siku wote tumekuwa
tunasimama kwa jina moja la Watanzania” Shaka Hamdu Shaka
“Mwezi Julai Rais Magufuli wakati
tunampokea Kisaki aliendelee kutusihi na kutuasa juu ya umoja na
mshikamano wetu sambamba na maelewano kati ya wakulima na wafugaji”
Shaka Hamdu Shaka
“Kiongozi au Serikali inapowakanya
wananchi wake kuhusu jambo fulani sio kama inawaogopa inawataka wajali
amani na watu wote waishi kwa mapatano katika jamii husika” Shaka Hamdu
Shaka
“Ikiwa kuna mtu anadhani
inawaogopa huko ni kujidanganya asitoke mtu akawashawishi mpingane na
dola, ishini kwa upendo huku kila upande ukiheshimu upande mwingine”
Shaka Hamdu Shaka
“leo mumenihakikishia kuwa jamii
hii mnamuunga mkono Rais Magufuli kwa mema na mazuri ya maendeleo
anayoyafanya kwa Taifa” Shaka Hamdu Shaka
“Niwaombe tumuunge mkono kwa
vitendo endeleni kuishi kwa kupendana na kushirikiana wafugaji na
wakulima ili kuepusha uhasama na madhara yasiyo ya lazima miongoni
mwetu” Shaka Hamdu Shaka
“Viongozi wa CCM na Serikali
inayotawala tunaowajibu wa kuwaweka pamoja mkiwa katika maelewano ili
mfanye kazi kwa pamoja kwa upendo na mshikamano na sio kuwagawa au
kuchochea migogoro katika kundi fulani” Shaka Hamdu Shaka
“Mara kadhaa hatutaki kuona
wananchi wakigombana au kuhasimiana, tabia ya kugombana, kupigana au
kubaguana sio sehemu ya silka, utamaduni wa watanzania” Shaka Hamdu
Shaka
#MorogoroYaKijaniInawezekana #TuwePamoja #TusikubaliKugawanyika
#Operationrekebishatabianamuelekeo#
0 comments:
Post a Comment