Sunday, September 1, 2019

MILA, SILKA NA UTAMADUNI WETU IWE CHACHU YA MAENDELEO YETU

Oleiboni Mtayani Simanga wa kijiji cha Kidui, kata ya Kilangali wilaya ya Wilaya ya Kilosa Leo amesimikwa rasmi kuwa Chief wa kimasai wa ukanda wa mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Dodoma.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na wazee wa kimila kutoka mikoa yote sita kikanda, viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wananchi mbali mbali pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ndugu Ruta Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, katibu, Katibu Mwenezi wa CCM Antony Muhando pamoja na viongozi kadhaa wa Chama na jumuiya.
Akitoa Salam za Chama Katibu wa CCM mkoa aligusia baadhi ya maeneo:
“Mila na tamaduni zetu ifike pahala sasa iwe ni sehemu ya kushamirisha maendeleo katika maeneo yetu” Shaka Hamdu Shaka
“Chief mpya ameainisha hapa kuwa atasimama upatikanaji wa elimu, kushirikiana na serikali katika kuhakikisha huduma za kijamii zinaimarika, kuhakikisha mnakuwa na maisha mazuri pamoja na nyumba za kisasa za kusihi” Shaka Hamdu Shaka
“Nchi yetu inabaraka toka enzi na asili wingi wa makabila yetu sio chochote kwetu umoja wetu na mshikamano tuliona ndio msingi wa Taifa letu mwisho wa siku wote tumekuwa tunasimama kwa jina moja la Watanzania” Shaka Hamdu Shaka
“Mwezi Julai Rais Magufuli wakati tunampokea Kisaki aliendelee kutusihi na kutuasa juu ya umoja na mshikamano wetu sambamba na maelewano kati ya wakulima na wafugaji” Shaka Hamdu Shaka
“Kiongozi au Serikali inapowakanya wananchi wake kuhusu jambo fulani sio kama inawaogopa inawataka wajali amani na watu wote waishi kwa mapatano katika jamii husika” Shaka Hamdu Shaka
“Ikiwa kuna mtu anadhani inawaogopa huko ni kujidanganya asitoke mtu akawashawishi mpingane na dola, ishini kwa upendo huku kila upande ukiheshimu upande mwingine” Shaka Hamdu Shaka
“leo mumenihakikishia kuwa jamii hii mnamuunga mkono Rais Magufuli kwa mema na mazuri ya maendeleo anayoyafanya kwa Taifa” Shaka Hamdu Shaka
“Niwaombe tumuunge mkono kwa vitendo endeleni kuishi kwa kupendana na kushirikiana wafugaji na wakulima ili kuepusha uhasama na madhara yasiyo ya lazima miongoni mwetu” Shaka Hamdu Shaka
“Viongozi wa CCM na Serikali inayotawala tunaowajibu wa kuwaweka pamoja mkiwa katika maelewano ili mfanye kazi kwa pamoja kwa upendo na mshikamano na sio kuwagawa au kuchochea migogoro katika kundi fulani” Shaka Hamdu Shaka
“Mara kadhaa hatutaki kuona wananchi wakigombana au kuhasimiana, tabia ya kugombana, kupigana au kubaguana sio sehemu ya silka, utamaduni wa watanzania” Shaka Hamdu Shaka
#MorogoroYaKijaniInawezekana #TuwePamoja #TusikubaliKugawanyika #Operationrekebishatabianamuelekeo#

No comments:

Post a Comment