Waziri wa Madini Doto Biteko (wa
pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck ( katikati), Naibu
Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia) na Afisa Madini
Mkoa wa Kimadini Kahama, Mhandisi Joseph Kumburu wakiangalia baadhi ya
Kaboni inayochenjuliwa katika Kituo cha Kuchenjua Dhahabu cha Jema
Afrika.
Afisa Madini Mkoa wa Kimadini
Kahama, Mhandisi Joseph Kumburu akizungumza jambo wakati wa ziara ya
Waziri wa Madini Doto Biteko katika kituo cha Kuchenjua Dhahabu cha Jema
Afrika. Wengine wanaosikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu
Tacleck na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo .
Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko
wakiteta jambo na Kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya
kukitembelea Kituo Kidogo cha Ununuzi wa Dhahabu Mwime.
Kamishna wa Madini Mhandisi David
Mulabwa ( kushoto) na Watalaam kutoka Tume ya Madini wakifuatilia jambo
wakati wa kikao cha ndani baina ya ujumbe wa Wizara na Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Madini Doto Biteko
akizungumza jambo wakati wa kikao cha ndani kabla ya kuanza ziara.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck.
……………………………..
Na Asteria Muhozya, Kahama
Waziri wa Madini Doto Biteko
ametoa Onyo la Mwisho la Kukifungia Kituo cha Uchenjuaji Dhahabu cha
Jema Afrika kilichopo Wilayani Kahama.
Hatua hiyo inafuatia kubainika
kwa jaribio la wizi wa dhahabu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa
kituo hicho kutaka kuiba dhahabu ya mteja.
Akizungumzia tukio hilo,
Waziri Biteko amewataka wamiliki wa kituo hicho kuandika barua ya kuweka
makubaliano na Serikali ya kutojirudia tena kwa vitendo vya wizi
kituoni hapo.
‘’Ni jicho la huruma tu
tukiwapeleka mahakamani mali zenu zitataifishwa. Tunajua mmewekeza
mitaji yenu na mna mikopo. Nilishamwambia mmiliki kuwa kituo chako
kina rekodi ya wizi. Rais anawapenda, anawapigania ili watanzania
wamiliki uchumi wa madini lakini mnamuangusha kwa kutofuata taratibu,’’
amesisitiza Waziri Biteko.
Amewatahadharisha wamiliki wa
vituo vya uchenjuaji nchini kuhusu wizi wote wa dhahabu unaofanyika na
kuwasisitiza kwamba, unafahamika na kuwataka wote wanaojihusisha na
vitendo hivyo kujiepusha na kwa wale wasiotaka kufanya kazi zao kwa
uaminifu watafute biashara nyingine.
Mbali na kutembelea kituo
hicho, pia, Waziri Biteko na ujumbe wake wametembelea Kituo Kidogo
cha Ununuzi wa dhahabu kilichopo katika eneo la Wachimbaji wadogo wa
Mwime ambapo amewapongeza kwa kufuata taratibu na Sheria na kuwataka
kufanya kazi zao kwa amani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck amesema Mkoa huo unahitaji wawekezaji lakini walio waaminifu.
Ameongeza kuwa, wizi na
udanganyifu katika kiwand cha uchenjuaji Jema Afrika ulibainiwa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama na kutumia fursa hiyo kuwatahadharisha wote
wasiofuata taratibu kuwa serikali inawaona na itawafikia.
Katika ziara hiyo, Waziri
Biteko pia ameongozana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga, Kamishna wa Madini
Mhandisi David Mulabwa na Watalaam kutoka Tume ya Madini.
Aidha, ziara hiyo imefanywa
wakati ambapo wizara na wadau wengine wa madini wanashiriki Maonesho ya
Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita
yanayotarajiwa kuhitimishwa Septemba 29, 2019.
Ziara hiyo imefanyika Septemba 28, 2019
0 comments:
Post a Comment