Mkuu wa Mkoa wa Manyara
ambaye pia ni Mmiliki wa timu ya Gwambina FC wa kwanza kushoto akiwa na
Mbunge wa Jimbo la Missungwi Mhe.Charles Kitwanga wa pili kutoka
kushoto wakifatilia mechi ya kirafiki kati ya wenyeji Dodoma FC na
Gwambina FC kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma timu zilitoka sare ya 1-1.
Wachezaji wa akiba wa
Dodoma Fc wakifatilia mtanange wa Kirafiki dhidi ya Gwambina Fc timu
hizo zilizotoka sare ya kufungana 1-1.
Wachezaji wa Gwambina wa
akiba akiwa kwenye benchi wakifatilia mechi yao dhidi ya Dodoma FC
uwanja wa Jamhuri timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Sehemu ya wachezaji
wakifajibika uwanjani katika mechi ya kirafiki kati ya wenyeji Dodoma FC
na Gwambina Fc kutoka wilayani Missungwi Mkoani Mwanza na timu hizo
zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Kocha Mkuu wa Gwambina
FC Fulgence Novatus,akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa
Jamhuri Dodoma zilipokutana na kutoshana bao 1-1.
Kocha Mkuu wa Dodoma FC
Mbwana Makata,akizungumzia mechi yao ya kirafiki dhidi ya Gwambina FC
ambapo timu hizo zilifungana bao 1-1 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
………………
Na.Alex Sonna
Timu za Dodoma FC na
Gwambina FC ya Misungwi kutoka jijini Mwanza wameshindwa kutambiana
baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika mchezo mkali na
wakusisimua kutokana na timu zote kucheza kiufundi na kukamiana sana,
ilishuhudiwa hadi kipindi cha kwanza kina malizika timu hizo zilikuwa
suluhu ya kila timu haikuweza kupata bao.
Gwambina ndio waliokuwa
wa kwanza kupata bao lililofungwa na mkongwe Jacob Masawe, baada ya
kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Dodoma FC Emanuel Mseja na kufanya
Gwambina kuongoza kwa bao moja bila.
Dodoma FC walisawazisha
dakika za mwisho kwa mkwaju wa penati, baada ya mchezaji wa Gwambina
kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, na mkwaju huo wa penati kufungwa
na Hamadi Kibopile.
Mchezo huo ulikuwa ni
wanne wa kirafiki kwa Dodoma FC na michezo yote imetoka sare, Gwambina
leo watashuka tena kwenye uwanja huo huo kucheza na Fountain Gate
inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment