Sunday, September 1, 2019

DODOMA FC YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA GWAMBINA FC MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA JAMHURI


Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mmiliki wa timu ya Gwambina FC wa kwanza kushoto  akiwa na Mbunge wa Jimbo la Missungwi Mhe.Charles Kitwanga wa pili kutoka kushoto wakifatilia mechi ya kirafiki kati ya wenyeji Dodoma FC na Gwambina FC kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma timu zilitoka sare ya 1-1.
Wachezaji wa akiba wa Dodoma Fc wakifatilia mtanange wa Kirafiki dhidi ya Gwambina Fc timu hizo zilizotoka sare ya kufungana 1-1.
Wachezaji wa Gwambina wa akiba akiwa kwenye benchi wakifatilia mechi yao dhidi ya Dodoma FC uwanja wa Jamhuri timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Sehemu ya wachezaji wakifajibika uwanjani katika mechi ya kirafiki kati ya wenyeji Dodoma FC na Gwambina Fc kutoka wilayani Missungwi Mkoani Mwanza na timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Kocha Mkuu wa Gwambina FC Fulgence Novatus,akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Jamhuri Dodoma zilipokutana na kutoshana bao 1-1.
Kocha Mkuu wa Dodoma FC Mbwana Makata,akizungumzia mechi yao ya kirafiki dhidi ya Gwambina FC ambapo timu hizo zilifungana bao 1-1 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

………………
Na.Alex Sonna
Timu za Dodoma FC na Gwambina FC ya Misungwi kutoka jijini Mwanza wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika mchezo mkali na wakusisimua kutokana na timu zote kucheza kiufundi na kukamiana sana, ilishuhudiwa hadi kipindi cha kwanza kina malizika timu hizo zilikuwa suluhu ya kila timu haikuweza kupata bao.
Gwambina ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mkongwe Jacob Masawe, baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Dodoma FC Emanuel Mseja na kufanya Gwambina kuongoza kwa bao moja bila.
Dodoma FC walisawazisha dakika za mwisho  kwa mkwaju wa penati, baada ya mchezaji wa Gwambina kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, na mkwaju huo wa penati kufungwa na Hamadi Kibopile.
Mchezo huo ulikuwa ni wanne wa kirafiki kwa Dodoma FC na michezo yote imetoka sare, Gwambina leo watashuka tena kwenye uwanja huo huo kucheza na Fountain Gate inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment