Waziri wa Nishati, Dkt.Medard
Kalemani(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kushoto)
wakibadilishana mawazo baada ya Waziri wa Nishati, kuwasili mkoani humo
kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani(kushoto) akipata maelezo ya namna kituo cha kupoza na kusambaza
umeme cha Singida, kinavyofanya kazi, kutoka kwa Meneja wa kituo
hicho, Mha. Malili Mipawa(kulia).
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kalemani, akikagua eneo itakaposimikwa moja ya transifoma katika kituo
cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard
Kalemani, akitoa maelezo kwa Mkandarasi na wasimamizi katika Ujenzi wa
upanuzi wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, baada ya
kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika kituo hicho.
Vibarua wakiendelea na kazi ya
ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida,
wakati Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, alipofanya ziara ya
kukagua shughuli za ujenzi katika kituo hicho.
Moja ya Transifoma kubwa ikiwa
imesimikwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida kwa
lengo kukiongezea uwezo kituo hicho hadi kufikia kV 400.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard
Kalemani( katikati) akikagua nguzo zilizo hifadhiwa katika kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Singida
……………
Na Zuena Msuya , Singida
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard
Kalemani amewagiza mameneja wa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)wote
nchini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wanasambaza kwa wateja nguzo
zote za akiba zilizohifadhiwa katika vituo na maeneo mbalimbali nchini.
Kalemani alisema hayo, Septemba
28,2019, baada ya kuona nguzo zaidi ya Elfu mbili zikiwa zimehifadhiwa
katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati wa ziara
yake ya kukagua ujenzi upanuzi wa kituo hicho kinachojengewa uwezo wa
kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti(kV) 400.
Dkt.Kalemani, alisema kuwa
hapendezwi kuona wateja wanalalamikia suala la ukosefu wa nguzo na
kushidwa kuunganishiwa umeme katika maeneo mbalimbali wakati kuna nguzo
zimerundwika mahali kwa ajili ya matumizi ya akiba.
“Wananchi wanahitaji nguzo kila
siku,mnawaambia hakuna nguzo, ajabu nguzo kama hizi zimehifadhiwa sehemu
mbalimbali mnadai ni za matumizi ya akiba,sasa akiba ya nini wakati
wananchi bado wanauhitaji , pia maeneo mengi nguzo zimeharibika
zinataka kubasilishwa, nawapa Mwezi mmoja zisionekane hapa na maeneo
mengine yote!”, Alisema Dkt.Kalemani.
Katika hatua nyingine, alimtaka
mkandarasi wa Kampuni ya KC International LTD inayotekeleza ujenzi wa
upanuzi wa Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida kuongeza
nguvu kazi ili kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ambao unatarajiwa
kukamilika mwezi Januari 2020.
Kazi ya ujenzi katika hatua ya
awali katika kituo hicho imekamilika na kufikia 95% ambapo pia tayari
wamekamilisha baadhi ya maeneo zitakaposimikwa transofoma kubwa nne
ambapo mbili kati ya hizo zitakuwa na uwezo wa 125 MVA kwa kila moja na
mbili nyingine zitakuwa na uwezi wa 250 MVA kila moja, pia kazi ya
kukamilisha ujenzi wa jengo la kuendeshea mitambo inaendelea .
Mradi huo ukikamilika utakuwa na
uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawat(MW) 432 ambapo kwa sasa mahitaji ya
umeme kwa Mkoa wa Singida ni MW 15 tu, hivyo kituo hicho kitaimarisha
upatikanaji wa Umeme wakutosha na wauhakika katika Mkoa huo na mikoa
iliyo karibu.
Kituo cha Kupoza na kusambaza
umeme cha Singida ndiyo kitakuwa kituo kikubwa na pia njia panda kubwa
ya kusambaza umeme kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia Mkoa wa
Shinyanga, Kanda ya Kaskazini kupitia Babati Mkoani Manyara, hadi
Namanga Mkoani Arusha na baadaye Nchini Kenya.
Gharama za upanuzi wa kituo hicho
ni Dola za Kimarekani milioni 60 sawa na Bilioni 130 za Kitanzania,
fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Shirika
la Maendeleo la Japan(JICA) pamoja na Fedha za ndani.
0 comments:
Post a Comment