Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa
Ismani, William Lukuvi (wa tano kushoto) wakizindua Upanuzi wa Kituo cha
Afya cha Idodi wilayani Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine pichani
kutoka kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mkoa wa
Iringa, Salim Abri, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mkuu wa
Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa,
Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia
ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi baada ya kuzindua Upanuzi wa Kituo
cha Afya Idodi wilayani Iringa , Septemba 28, 2019. Kulia ni Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikata utepe kuzindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi Wilayani
Iringa, Septemba 28, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, Mwenyekiti wa CCM wa
Wilaya ya Iringa, Costantino Kihwele, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa
Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi, Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ismani, William
Lukuvi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda, Mke wa Waziri
Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa
Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa na Kulia
ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na
Mkewe Mary wakimpongeza, Bibi Chipe Ngubi ambaye amejifungua mtoto wa
kiume Greyson wakati walipozindua Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Idodi
wilayani Iringa na kutembelea Wodi ya Mama na Mtoto, Septemba 28, 2019.
Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa
Ismani Wiliam Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Mkewe Mary wakitazama ngoma wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji
cha Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadahara, Septemba 28,
2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi,
ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati walipowasili kwenye uwanja wa
kijiji cha Idodi wilayani Iringa kuhutubia mkutano wa hadhara, Septemba
28, 2019.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani, William Lukuvi
akiwasalimia wapiga kura wake kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Idodi wilayani
Iringa, Septemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Mkewe Mary (aliyekaa wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa mkao wa Iringa na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya
Iringa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa
hadhara katika kijiji cha Idodi, Septemba 29, 2019. Kushoto (aliyekaa)
ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa
Ismani, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment