METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 20, 2019

Dkt Tulia Ackson azindua Maadhimisho ya kutangaza Utalii Nyanda za Juu Kusini






Leo Septemba 20, 2019 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya kutangaza Utalii Nyanda za Juu Kusini.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ijulikanayo kama "Karibu Kusini kwa Utalii na Uwekezaji" yanafanyika katika Viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa kwa siku tatu mfululizo.

Akitoa hotuba yake Dkt Tulia amewasihi viongozi na wadau mbalimbali wa Mikoa ya Kusini kuwa wabunifu zaidi katika kubuni na kuibua vivutio ambavyo vinajitofautisha na maeneo mengine na havipatikani mahali popote pale isipokuwa katika Mikoa hiyo.

“Ni wazi kuwa Utalii ni moja ya sekta inayochangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa hivyo huu ni wakati wetu kuwekeza na kuboresha sekta hii” Alisema

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com