METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 3, 2019

Dkt. Kalemani: Mwanakijiji kuweka umeme ni lazima si hiari


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akiwa ameshika mkuki huku amevaa mavazi maalum baada ya kusimikwa kuwa Chifu wa Kijiji cha Ihalula, kutoka kwa mmoja wa wazee wa kimila( aliyesimama kulia), baada kuwasha umeme katika kijiji hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( wa pili kulia) akitoa maelekezo baada ya kutembelea chumba kujifungulia akina mama wajawazito katika Kituo cha Afya cha Ihalula, katika halmashauri ya wilaya ya Njombe, mkoani njombe,baada ya kuwasha umeme katika zahanati hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto) akigana na Mbunge wa Wanging’ombe, Gerson LWENGE( kulia) baada ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Itombololo, wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( katikati) akikata utepe kushiria kuwasha umeme katika moja ya shule za msingi katika Kijiji cha Saja, wilayani ya Wanging’ombe mkoani Njombe.
***************
Na Zuena Msuya, Njombe
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amesema zoezi la mwakijiji yeyote kuunganishiwa umeme ni lazima siyo hiari kwa kuwa kila mtanzania hasa walio vijijini wanamudu gharama ya kuunganishiwa umeme kutokana na kiwango cha gharama kilichopangwa na serikali.
Dkt.Kalemani alisema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme vijijini(REA) ili uweze kuwafikia wananchi wote walioko vijijini ambao wanatakiwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kuunganishwa na huduma hiyo.
Dkt.Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika vijijini vinne ambavyo ni Ihalula, Itombololo, Itowo na Saja vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya Njombe na Wanging’ombe mkoani Njombe, Septemba 2,2019.
Kwa mujibu wa Dkt.Kalemani, Serikali iliangalia hali ya uchumi kwa wananchi wake wote hasa wanaoishi Vijijini na kujiridhisha kuwa kila mlengwa anauwezo kwa kuchangia shilingi 27,000/= ikiwa ni gharama nafuu ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa gharama zingine za kutekeleza mradi huo zinalipwa na serikali.
Alifafanua kuwa zoezi kuunganisha umeme kwa kila nyumba ya mwanakijiji anaeishi kijijini ni lazima kwa sababu Mradi wa Usambaji Umeme Vijijini( REA) unaunganisha nyumba za aina zote na maeneo yote ya vijijini bila kujali itikadi za Kisiasa, Imani za Dini, wala Kabila.
Aliendelea kusisitiza kuwa, hapo baadaye serikali itafanya zoezi la kukagua nyumba moja baada ya nyingine zilizopo vijijini kufuatilia zoezi la uunganishwaji wa umeme kwa wanavijiji, na endapo watabaini kuwa mwakijiji ameshindwa kuunganisha huduma hiyo bila sababu ya msingi, basi itamlazimu kuuza mifugo au mazao ili kupata shilingi 27,000/= ikiwa ni gharama ya kunganisha umeme kwa lazima.
“Zoezi la kuweka umeme katika kila nyumba vijijini ni lazima siyo hiari kama mnavyodhani, serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza mradi wa ( REA),pia ni nia ya kuwasogezea huduma bora na za msingi kwa maendeleo ya wananchi wake, ambao na wao watachangia gharama ndogo: Sasa usipoweka umeme tutakuja kuuza chochote unachozalisha nyumbani kwako tukulipie huduma hii”. Alisema Dkt.Kalemani.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com