![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-A-1-1024x683.jpg)
Afisa Biashara wa Taasisi ya
Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine
Mungo(wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano
wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) uliofanywa
kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu
za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo
yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-B-1024x640.jpg)
Afisa Uhusiano wa wa Baraza
laTaifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Edward Kessy
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani )
uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa
rasmi ya katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe
14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-C-1024x683.jpg)
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la
Bariadi, Bw. Shadrack Daudi (wa pili kushoto) akizungumza akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019
Mjini Bariadi kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii
yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa
20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-D-1-1024x683.jpg)
Afisa kutoka Benki ya Tanzania
(BOT), Bi. Edista Njau (kushoto) akizungumza akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani ) uliofanyika leo Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi
kwa lengo la kutoa taarifa rasmi ya maonesho ya tatu ya mifuko/programu
za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo
yameanza tarehe 14 Oktoba, 2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-E-1-1024x683.jpg)
Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya
mitaji kutoka katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi wakitoa
ushuhuda kwa waandishi wa habari namna mifuko hiyo ilivyowasaidia kupata
mitaji, wanufaika hao wamehojiwa katika banda la Benki Kuu ya Tanzania,
katika maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya
kifedha vya kijamii yanayoendelea ambayo yameanza tarehe 14 Oktoba,
2019 na yatahitimishwa 20 Oktoba, 2019 Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
…………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii
yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo
washiriki kutoka taasisi za Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya
uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya kijamii (VICOBA) wanatarajiwa
kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa
habari Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy ambao
ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya
kanda ya ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha
na programu mbalimbali.
“Maonesho haya yameanza Oktoba
14, 2019 na yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu na yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa
wingi ili waje wajionee huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi
vya kijamii,” alisema Kessy.
Afisa Biashara wa Taasisi ya
Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo
ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kujua huduma zao, huku
akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango mkakati wa miaka mitano
ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia 235,000 kwa kudhamini
mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .
Kwa upande wake Meneja wa
Benki ya Posta Tanzania tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema
benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC na PASS imetoa mikopo ya vikundi
mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na visivyo rasmi, wafanyabiashara,
hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi kujionea fursa hizo ambazo
zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naye mnufaika wa mikopo ya
mifuko ya uwezeshaji, Bw. Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika
cha Msingi kutoka Kahama, ametoa wito kwa wananchi kufika katika
maonesho hayo ili waweze kuona fursa za upatikanaji wa mikopo kupitia
mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha huku akieleza kuwa
hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.
“Natoa wito kwa wajasiriamali
wadogo au vyama mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze
namna ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli za kiuchumi,
niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo, tunaipata kwa wakati na
Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu kurejesha mikopo,”
alisema Nyambi.
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.
0 comments:
Post a Comment