METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 10, 2021

RC MAHENGE AWATAKA WAKANDARASI KUMALIZA MIRADI YA MADARAJA KABLA MSIMU WA MVUA HAUJAFIKA

Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akiwa na viongozi mbalimbali na waandishi wa habari  wakati wa ukaguzi wa  ujenzi wa daraja katika kata ya Msingi wilyani Mkalama mkoani Singida 

Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akitoa maelekezo kwa meneja wa TANROAD Mhandisi Deus Masige  mkoa singida baada ya kutembelea ujenzi wa daraja, pembeni ni Mkuu wa wilaya ya mkalama mhe. Sophia Mfaume Kizigo

Diwani wa Kata ya  msingi mhe.Amri juma akitoa shukrani kwa serikali kwa niaba ya wananchi kutokana na ujenzi wa daraja hilo.

Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka TANROAD kumaliza haraka ujenzi wa daraja unaoendelea katika Kata ya Msingi Wilayani Mkalama Mkoani humo ili kurahisisha mawasiliano  katika maeneo mbalimbali  kabla msimu wa mvua haujaanza.

Dkt. Binilith Mahenge ametoa maelekezo hayo leo tarehe 10.08.2021 alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja lililopo   Kata ya Msingi wilaya ya Mkalama ambapo amesema daraja hilo likikamilika litweza kuhudmia mikoa ya Mwanza Simyu na Manyara.

Aidha amewapongeza viongozi wa TANROAD Mkoani hapo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo na kuwataka kuhakikisha kwamba daraja likamilika kwa ubora na muda uliopangwa.

Hata hivyo RC amebainisha kwamba kumalizika kwa ujenzi wa daraja hilo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10.9 na linatakiwa kukamilika ifikapo tarehe 30.10.2020. 

Aidha Mhe. Dkt. Mahenge amewapongeza Viongozi wa TANROAD  kwa usimamizi mzuri pamoja na changamoto za mvua kwa msimu uliopita lakini kazi imeendelea kuwa nzuri. 

Amesema kukamilika kwa daraja hilo kutahamasisha  kwa kiasi kikukbwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na  taifa kwa ujumla.

“Nimefahamishwa kwamba dararaja hili linaunganisha mikoa ya Simyu ,Mwanza, Manyara na kwa mkoa wa Singida linaunganisha Wilaya ya Mkalama na Iramba, ni matumaini yangu kwamba shughuli za uchumi zitaimarika sana kwa mtu momoja na Taifa kwa ujumla wake” Alisema Dkt. Mahenge.

Awali akimkaribisha RC Mkuu Wilaya ya Mkalama Mhe.  Sophia Mfaume Kizigo amesema daraja hilo ambalo ni kiungo muhmu cha wilaya ya Mkalama na Iramba litawasidia wananchi wa maeneo hayo kuendesha shukughuli za kila siku kwa ufasaha kutoka eneo moja kwenda jingine.

Aidha ufanikishwaji wa daraja hilo utasababisha barabara nyingine zinazounga wilaya na mikoa mbalimbali kujengwa kwa kiwango cha lami alisistiza Mhe.  Sophia

Naye Diwani wa Kata ya Msingi wilayani hapo Mhe. Amri Juma  ameishukuru serikali kwa jitihada za kufanikisha ujenzi wa daraja hilo na mengine madogo ya nayojengwa na TARURA katika Kata hiyo kwamba ni Ishara ya mabadiliko makubwa ya kiutendaji unaofanywa na serikali ya awamu ta sita.

Naye Mhandisi Deus Masige  Meneja wa TANROAD mkoani Singida amesema daraja linaurefu wa mita 100 na midomo ya kupitisha maji  mnne (4)  ambapo limefikia asilimia 67 na linatumia fedha za ndani.

Ujenzi wa daraja hilo ulitegemewa kumalizika   tarehe 11/12 /2021 lakini kutokana na changamoto za mvua kwa msimu uliopita halikuweza kumalizika kwa wakati.

Mwisho Mhandisi Masige amehakikishia Mkuu wa mkoa kwamba pamoja na changamoto zilizojitokeza lakini ujenzi wa daraja hilo utakamilika ifikapo 30/10/2021.

Katika hatua nyingine Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka wananchi wa Mkalama na maeneo mengine kujikinga na ungojwa wa covid 19 na kuendelea kupata chanjo ambazo serikali imeshazisambaza maeneo mbalimbali mkoani hapo.

Amesema Mkoa umepokea chacho Zaidi ya 30,000 ili wananchi waweze kupata  chanjo hizo ambazo serikali imejiridhizsha kwamba ni salama kwa afya ya watu wake.

Aidha Mhe. Dkt. Mahenge amewaagiza wakuu wa wilaya zote mkoani hapo kuendelea kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya korona kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Amewataka madiwani kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu misongamono ambayo sio ya lazima ili kuepuka usambazaji wa ugonjwa huo endapo mtu mmoja atakuwa ameathirika.

Naye Mzee Aroni Msindye Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa chama cha mapinduzi ccm wilayani hapo ameiomba serikali kusogeza karibu vituo vya kupatia chanjo ili wazee waweze kufika kw urahisi.

Mzee Aroni amebainisha kwamba wazee kwa sasa wanapata changamoto ya umbali hivyo wengi kushindwa kupata chanjo hiyo.

Imeandaliwa na  

Afisa Habari 

Mkuu wa Mkoa Singida 

Mwisho.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com