Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelekezo kuhusu
mfumo wa matumizi ya simu za mezani kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakati wa kutembelea mabanda
mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa Mawaziri wa sekta za Tehama,
Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC) leo Ijumaa Septemba 20, 2019.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
wa pili (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Sekta za
Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewakutoka Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada ya kufunga mkutano huo leo Ijumaa
Septemba 20, 2019.
(PICHA NA MAELEZO)
************************************
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
20.9.2019
MAKAMU wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka Mawaziri wa Sekta za TEHAMA,
Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini
mwa Afrika (SADC) kuyapa uzito maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wao
kuleta ustawi wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Ukanda
huo.
Akifunga Mkutano wa Mawaziri wa
SADC wa sekta za TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa leo Ijumaa
(Septemba 20, 2019) Jijini Dar es Salaam, Balozi Seif alisema ajenda na
maazimio ya mkutano mkutano huo ni maeneo muhimu yatakayoweza
kuharakisha kasi ya ukuaji wa uchumi na biashara kiuchumi katika ukanda
wa SADC.
Balozi Idd alisema miongoni mwa
maeneo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na ukuaji wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo kwa sasa ukuaji wake umekuwa
ni sehemu muhimu katika maendeleo ya kiuchumi ndani ya Jumuiya hiyo
ikienda sambamba Mpango Mkakati Wa Maendeleo wa ya Miundombinu ya
Kikanda jumuiya hiyo wa mwaka 2019-2023.
Aidha Balozi alisema malengo ya
Tanzania ni kuhakikisha Jumuiya hiyo inakuwa na mshikamano na nguvu ya
pamoja katika kuondoa na kukabiliana na vikwazo mbalimbali
vinavyosababisha ukuaji hafifu wa maendeleo ya kiuchumi katika SADC
vikwazo vya biashara ya mipakani vilivyopo baina ya Nchi na Nchi ndani
ya Jumuiya hiyo.
“Mkutano huu umekuwa muhimu kwa
ustawi wa Jumuiya ya SADC, wananchi wa mataifa yetu wanatarajia kupata
unafuu na kutengeneza fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo masoko,
biashara na ajira na kwa kufanya hivi tutatekeleza Mipango Mikakati
tuliyojiwekea katika kuinua uchumi wa mataifa yetu ndani ya Jumuiya”
alisema Balozi Idd.
Kwa mujibu wa Balozi Seif alisema
sekta za TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hali pia zina mchango
mkubwa katika kuleta mageuzi ya uzalishaji mali na ufanyaji biashara
ndani ya Jumuiya ya SADC na hivyo kuzitaka Nchi wanachama kuweka mkazo
katika kubuni mipango madhubuti itakayowahakikishia inakuza na
kuimarisha miundombinu iliyopo.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alisema katika Mkutani
huo, Mawaziri wa sekta hizo wamekuwa na majadiliano mapana yaliyoweza
kujadili kwa kina changamoto mbalimbali zilizopo katika Nchi wananchama
wa Jumuiya hiyo na kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Aliitaja moja ya changamoto hiyo
kuwa ni pamoja na vikwazo vya ufanyaji biashara katika mipaka baina ya
Nchi hizo na kueleza kuwa kwa pamoja wamejipanga kuhakikisha kuwa
wananachi wa Mataifa hayo wanakuwa na fursa ya kutembeleana na kuweza
kufanya biashara baina yao bila vikwazo vya kisheria na kisera.
“Mkutano huu umekuwa muhimu sana
kwa manufaa ya wananchi wetu kwani umeweza kuweka mikakati ya pamoja
itakayosaidia wananachi wetu kupata unafuu wa gharama katika mfumo mzima
wa ufanyaji biashara uliopo katika jumuiya yetu” alisema Waziri
Kamwelwe.
Kamwelwe alisema mkutano huo pia
ni sehemu muhimu iliyowapa fursa wajumbe wa kuweka mikakati ya pamoja ya
njia bora zitakazowezesha kuzinufaisha Nchi wanachama kuweza kutumia
fursa za ukuaji wa teknolojia katika kutengeneza fursa ya ukuaji wa
sekta za kijamii na kiuchumi ndani ya jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment