WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania
imeendelea kuchukua hatua za makusudi kwa ajili ya kuwawezesha
Watanzania washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao, ikiwa
ni pamoja na kubadilisha sera na sheria zinazohusisha sekta mbalimbali
ikiwemo mafuta, madini, bima na ununuzi wa umma.
Amesema
lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanapewa
kipaumbele kwenye ajira, ununuzi wa bidhaa na huduma zao, uongezaji wa
ujuzi na uhaulishaji wa teknolojia kupitia miradi hiyo ya kimkakati
inayotekelezwa nchini.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 20, 2019) wakati
wa akifungaKongamano la Taifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi
ya Kimkakati ya Uwekezaji (Local Content) lililofanyika kwenyeukumbi
wa LAPF jijini Dodoma.
“Nyote
mtakubaliana nami kuwa ushiriki wa wananchi katika uchumi wa Taifa lao
ni suala linalopewa kipaumbele katika nchi nyingi duniani kwa kuwa
linachangia katika kukuza uchumi wa nchi husika.”
Amesema Serikali
imeendelea kutoa kipaumbele kwenye huduma mbalimbali ikiwemo bima,
huduma za benki, sheria na uhandisi. “Vilevile, mikataba mbalimbali ya
ujenzi wa miundombinu pia imetoa kipaumbele kwenye ajira za Watanzania
pamoja na bidhaa na huduma ambazo zinapatikana hapa nchini.”
Waziri Mkuu amesema Serikaliya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeweka dhamira
ya dhati ya kutekeleza Sera ya Viwanda inayolenga kuipeleka nchi katika
uchumi wa kati ifikapo 2025.
Amesema
jitihada za makusudi zimeendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kusimamia
na kufanikisha utekelezaji wa malengo mbalimbali pamoja na Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi 2015/2020.
Pia, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2017/2020/2021 ambao pamoja na mambo mengine una lenga kuimarisha
upatikanaji wa stadi zinazohitajika viwandani, na stadi kwa ajili ya
shughuli nyingine za uzalishaji na utoaji huduma.Amesema
dhana ya ushiriki wa wananchi (Local Content) ni mojawapo ya nyenzo
muhimu itakayowezesha Tanzania kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema iwapo bidhaa na huduma za Kitanzania zitatumika
kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini viwanda
vya ndani vitakua, malighafi zinazopatikana nchini zitapata soko la
uhakika, ajira zitaongezeka na hivyo uchumi wa nchi utakua kwa kasi.
“Hakuna
nchi yoyote ile duniani inayoweza kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo na
kufanikiwa bila ya kuweka dhamira na jitihada za makusudi za kuhakikisha
kunakuwa na mazingira wezeshi kwa wananchi wake kushiriki ipasavyo
kwenye shughuli za kiuchumi.”
Amesema
Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha mazingira ya kisera na kisheria yanaboreshwa kwa kuzingatia
maslahi ya wananchi wake, hivyo Serikali itafanya kazi kwa karibu na
sekta binafsi ili kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa kwa kuwa sekta
binafsi ina mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi na kutoa ajira
kwa Watanzania.
Waziri
Mkuu amesema tarehe 21 Julai 2016, wakati alipozindua Kongamo la Taifa
la Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati aliagiza
kutengenezwa kwa Mwongozo wa Taifa wa Ushiriki wa Watanzania katika
Uwekezaji (National Multi-sector Local Content Guidelienes). Mwongozo
huo umekamila na ameuzindua leo pamoja na tovuti ya Miradi ya Kimkakati
na Uwekezaji.
Tovuti
hiyo, itakuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya kimkakati, fursa
zilizopo kwenye miradi hiyo pamoja na mipango na mikakati mbalimbali
kuhusu masuala ya ushiriki wa wananchi kwenye miradi hiyo. Pia
itawezesha kujenga uelewa wa umma kuhusu ushiriki wa wananchi kwenye
miradi ya kimkakati na kufahamu changamoto zinazowakabili Watanzania
katika ushiriki kwenye miradi mbalimbali ili kuzipatia suluhisho
changamoto hizo.
Hivyo,
Waziri Mkuu ameagiza Mwongozo wa Taifa wa Kisekta wa ushiriki wa
Watanzania usambazwe kwa wadau mbalimbali ili waweze kufahamu majukumu
walionayo katika kuwawezesha Watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi.
“Tujenge utamaduni wa kufuatilia tovuti ya Serikali ya miradi mikubwa
ya kimkakati na uwekezaji ili kutambua fursa za kibiashara.
Kongamano
hilo limehudhuriwa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Sera, Bunge, Ajira,
Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Dkt. Bilnith Mahenge, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi KiuchumiBeng’i Issa.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Salum Shamte,
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi KiuchumiDkt.
Festus Limbu pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi,
wafanyabiashara, wanatlaaluma, watafiti, asasi za kiraia na vikundi
mbalimbali vya wajasiriliamali.
0 comments:
Post a Comment