
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi akiongea kwa furaha na
wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku
kadhaa. Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt
Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi,
ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa
Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa
ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe
Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi
Dar es salaam alikopatiwa matibabu Pia amewashukuru Madaktari wa
KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya
kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na
Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius
Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya
kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019. Mhashama
Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika
Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa
upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru
Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa
ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa
matibabu. Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa
MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu.
Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa
kumuombea.
PICHA NA ISSA MICHUZI
0 comments:
Post a Comment