Waziri Mkuu wa jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh Kasimu Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe wakati akifafanua jambao
katika eneo la msavu mahali ilipotokea ajali ya moto.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa Akimbatana Viongozi Mbalimbali
Wa Kiserikali Katika wakati alipokagua eneo la ajali Msamvu Mkoani
Morogoro.
Mabaki ya Lori la mafuta lililopinduka jana asubuhi mjini Morogoro na kulipuka moto.
Wananchi waliojitokeza katika
uwanja wa shule ya sekondari morogoro kwa ajili ya utambuzi wa miili ya
ndugu zao waliopata ajali ya lori la mafuta lililolipuka katika eneo la
Msavu.
……………………………………………………..
FARIDA SAIDY MOROGORO
Waziri Mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Kasimu
Majaliwa ameunda tume itakayochunguza chazo cha ajali ya lori
lililolipuka na kuwaka moto.
Tume hiyo imeundwa leo jumapili
Agosti 11,2019 ili kuchunguza kama kuna mamlaka au mtu yeyote ambaye
hakuwajibika vya kutosha katika kuchukua hatua kutokana na ajali hiyo na
imetakiwa kukamilisha uchunguzi huo ijumaa agosti 16 mwaka huu.
‘’Ninaunda tume ianze kuchunguza
kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa
sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha
kufanya.’’amesema Majaliwa.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi
Agosti 10, 2019 maeneo ya , Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la
mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya wananchi kuanza
kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo..
Aidha mpaka sasa Waziri mkuu
amesema kuwa watu waliofariki ni 69, na majeruhi zaidi ya 66 ambapo Mh
Kassim Majaliwa amewataka wanahabri kutokutoa takwimu zisizo sahihi
kwani swala hilo linawatia hofu watanzania.
‘’Naogopa msije mkaingia kwenye
sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni takwimu sahihi kutoka vyombo
vinavyohusika na za Mkuu wa Mkoa” Amesema Mh. Kassim Majaliwa.
0 comments:
Post a Comment