Mkurugenzi wa utetezi na maboresho
wa mtandao wa haki za binadamu Fulgence Massawe ,akizungumza wakati wa
mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha
baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu
na wananchi.
Mkurugenzi wa shirika la Faraja
ambalo pia linafanya kazi na watoto wa mitaani pia ni mchechemuaji wa
jamii, Bi.Philipina Labia,akifafanua jambo wakati wa mdahalo
ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na
wananchi
Mhadhiri msaidizi wa chuo cha
Mtakatifu John,Ntebi Elkana,akichangia mada wakati wa mdahalo
ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na
wananchi
Katibu Mkuu klabu ya Haki za
Binadamu Chuo cha Mtakatifu John Bw.John Gerald ,akichangia mada wakati
wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha
baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu
na wananchi
Mwanafunzi kutoka Chuo cha
Mtakatifu John,Azimu Ramsey,akiongea wakati wa mdahalo ulioandaliwa na
kituo cha haki za binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi
Mwenyekiti klabu ya haki za
binadamu Chuo cha Mtakatifu Joh,Bw.Emmanuel Ponda,akielezea jambo wakati
wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na kushirikisha
baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi kwa karibu
na wananchi
Picha ya pamoja na wanaharakati
pamoja na washiriki wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za
binadamu na kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
yanayofanya kazi kwa karibu na wananchi.
……………
Na.Alex Mathias,Dodoma
Baadhi ya wadau na watetezi wa
haki za binadamu wameomba kutolewa kwa elimu ya kutosha kwa wananchi
kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi
karibuni kote hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma
wakati wa mdahalo ulioandaliwa na kituo cha haki za binadamu na
kushirikisha baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya
kazi kwa karibu na wananchi.
Wadau hao akiwamo Ntebi Elkana
mhadhiri msaidizi wa chuo cha Mtakatifu John, amesema kuna haja kwa
serikali na wadau wengine kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi waelewe
ili washiriki katika uchaguzi huo kikamilifu.
“Bado kuna haja ya kutoa elimu ya
kutosha kwa watu wajitambue kwa sababu watu wa hali ya chini bado
hawajafikiwa na elimu kuhusu huu uchaguzi wa serikali za mitaa ili
washiriki kikamilifu” amesema Elkana.
Amesema bado kuna haja ya kutoa
elimu ya uraia kwa jamii kwa sababu elimu ya uraia haijawafikia
kikamilifu wananchi amebainisha kuna idadi kubwa ya watu hawafikiwi na
elimu hiyo.
“Hii elimu ya uraia ifikiwe kwa
ukubwa wake sawa tutawafundisha katika vyuo vikuu lakini ukiangalia kuna
namba kubwa ya wanaoishia elimu ya chini hawafiki elimu ya juu hii
elimu ya uraia wanaikosa” amesema.
Kwa upande wake Faraja Kikoti
ambaye ni mhitimu ya Chuo cha Mtakatifu John, amesema habari na elimu
hiyo haiwafikii wananchi wa hali ya chini kwa sababu ya ubovu wa
miondombinu maeneo ya vijijini kuna baadhi ya wataalamu hawafiki huko na
wananchi kukosa kabisa elimu hiyo.
Nae mkurugenzi wa shirika la
Faraja ambalo pia linafanya kazi na watoto wa mitaani ambaye pia ni
mchechemuaji wa jamii, Philipina Labia, amesema kuna baadhi ya mashirika
ya kiraia yanayopata ruzuku kwa ajiri ya kutoa elimu kwa raia ni wajibu
wao kufika hadi ngazi za chini kabisa.
“Haya mashirika yanayopata ruzuku
kwa ajiri ya kutoa hii elimu inabidi wafike hadi ngazi za chini kabisa
bila kujali kuna vikwazo gani wanakutana navyo, lazima wahimizwe elimu
ifike ya kutosha kwa jamii” amesema Philipina.
Amesema bado katiba yetu ina
mapungufu na hivyo kuna haja ya kuifanyia mabadiliko kama ambavyo
mchakato ulianza amebainisha kuwa bado kuna wananchi hawana elimu ya
uraia na hata katiba iliyopo haijawafikia wananchi kiasi cha kujua haki
zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
utetezi na maboresho wa mtandao wa haki za binadamu Fulgence Massawe,
amesema elimu ya kutosha ipelekwa wa jamii kwani uchaguzi wa serikali za
mitaa ni muhimu kuliko uchaguzi mkuu.
Kwani viongozi wanaochaguliwa ndio
wanaenda kufanya kazi moja kwa moja na wananchi na elimu isipotolewa ya
kutosha na wakachaguliwa viongozi wasiofaa ni hatari kwa jamii hayo
kwa sababu itakosa matumaini kabisa.
0 comments:
Post a Comment