Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela (aliyevaa kofia nyeusi) akifanya mazoezi na wananchi
wa Wilaya ya Songwe mapema leo kabla ya kuzindua Mkwajuni Jogging Club.
Wanafunzi na wanawake
waliojitokeza wakiendelea na mazoezi mapema leo Wilayani Songwe kabla ya
uzinduzi wa Mkwajuni Jogging Club.
Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe Mercy
Mollel (wa kwanza kushoto) akifanya mazoezi na wananchi wa Wilaya ya
Songwe mapema leo kabla ya uzinduzi wa Mkwajuni Jogging Club.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe
Eliniko Mkola (aliyevaa tracksuit ya bluu) akifanya mazoezi na wananchi
wa Wilaya ya Songwe mapema leo kabla ya uzinduzi wa Mkwajuni Jogging
Club.
******************
Wanafunzi wawili kutoka Wilayani
Songwe wanatarajiwa kupewa nafasi ya Kupanda Mlima Kilimanjaro mwezi
ujao ikiwa ni sehemu ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Kifo cha baba Taifa
hayati J. K. Nyerere itakayofanyika Oktoba 14 mwaka huu Mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela ametoa ahadi hiyo mapema leo wakati wa mazoezi ya
viungo na Uzinduzi wa Club ya Mkwajuni Jogging club ya Wilayani Songwe.
Kabla ya uzinduzi huo, Brig. Jen.
Mwangela amewaongoza wananchi wa Wilaya ya Songwe kufanya mazoezi ya
kukimbia yaani Jogging kwa takribani kilomita saba pamoja na kufanya
mazoezi mbalimbali ya viungo.
Aidha amesema Mkoa wa Songwe
tayari una jumla ya vijana 11 ambao wameshapanda Mlima Kilimajaro kama
sehemu ya kuonyesha uzalendo wao na vijana hao ni wale ambao hupenda
kufanya mazoezi.
“Wanafunzi fanyeni mazoezi kwa
ajili ya afya ya mwili na akili pia tutachagua wanafunzi wawili ambao
watapewa mazoezi na wana Kimondo Jogging Club, mazoezi hayo yanahusisha
kupanda Mlima Rungwe angalau mara mbili ndipo muweze kupanda Mlima
Kilimanjaro, nitajitahidi tupate wanafunzi wa kike na wa kiume
mtuwakilishe”, Bri. Jen. Mwangela
Amesisitiza kuwa mazoezi ni mazuri
kwa afya na ni ajira, pia amewapongeza wananchi wa Waliojitokeza
kushiriki mazoezi hayo huku akiwasisitiza kuendeleza utaratibu wa
kufanya mazoezi mara kwa mara.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya amesema kila mtu anapaswa kufanya mazoezi
angalau kwa muda wa dakika 30 kila siku ili kujiepusha na magonjwa
yasiyoambukiza ambayo kwa sasa husababisha vifo kwa zaidi ya asilimia
30.
Dkt Kagya amesema kufanya mazoezi
huondoa mafuta yasiyotakiwa mwilini, husaidia mzunguko wa damu kufanya
kazi vizuri na ukifanya mazoezi kwa muendelezo mwili utaweza kuepuka
magonjwa ya mara kwa mara.
Bi Shuhudia Huseni Musa mkazi wa
Mkwajuni Wilayani Songwe amesema amefurahia kufanya mazoezi licha
kupata maumivu ya viungo kwakuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya
mazoezi kama hayo.
Amesema kwa kufanya mazoezi kila
siku kunaweza kusaidia kujikinga na magonjwa kama vile shinikizo la
damu, kisukari, uzito uliozidi hivyo anawashauri watu wazima hususani
wanawake wawe na tabia ya kufanya mazoezi.
0 comments:
Post a Comment